Jeshi la Polisi mkoani Arusha
jana asubuhi lilituliza vurugu za viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya
CCM (UVCCM) mkoani hapa, waliokuwa wakigombea ofisi.
Vurugu hizo
ziliibuka hadharani jana baada ya kuwapo taarifa za mgogoro wa chini kwa
chini uliodumu kwa kwa miezi miwili, kati ya makundi mawili
yanayokinzana kiuongozi.
Mgogoro huo ulielezwa kukolezwa na uhamisho wa
Katibu wa UVCCM Mkoa, Ezekiel Mollel kwenda makao makuu, huku katibu
mpya aliyepelekwa kuchukua nafasi hiyo akikwama kukabidhiwa kwa siku
tatu sasa.
Katibu huyo mpya Saidi Goha, jana alitaka kuingia ofisini
lakini alikumbana na kigingi cha kundi linalomuunga mkono Mollel
lililofunga mlango kwa mnyororo. Kutokana na vurugu za jana, polisi
wanamshikilia
mwenyekiti wa miradi ya jumuiya hiyo, Phillemon Ammo pamoja na Mollel.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema: “Ni kweli tumemkamata lakini
nina ugeni wa Serikali (wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan), naomba
nitoe taarifa baadaye,” alisema Mkumbo.
Lengai Ole Sabaya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, alisema anapinga na kulaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa umoja huo kufunga ofisi hizo kinyume na taratibu.
Lengai Ole Sabaya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, alisema anapinga na kulaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa umoja huo kufunga ofisi hizo kinyume na taratibu.
Mollel anadai uhamisho wake ni njama za
kupoteza ushahidi wa baadhi ya tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya
fedha kwenye jumuiya hiyo, hivyo hatokwenda popote.
Anasema yeye anatekeleza maagizo ya kamati ya utekelezaji ya kusimamia mali za chama,
kwani katika kipindi cha miezi miwili ameokoa zaidi ya Sh30 milioni
ambazo zilikuwa zinaingia mifukoni mwa watu wachache.
“Tuna maduka
hapa, waliopangishwa wanalipa zaidi ya Sh300,000 lakini chama kinapata
chini ya Sh50,000 kwa duka kama kodi ya mwezi sasa tumetaka wenye maduka
kulipa moja kwa moja UVCCM na siyo kwa watu wa kati na hapa ndipo
chanzo cha mgogoro,” alisema.
Kutokana na vurugu hizo zilizoibuka jana asubuhi, Sekretarieti ya UVCCM imeamua kumsimamisha kazi bwana Ezekiel Mollel.
Kaimu Katibu wa UVCCM,
Shaka Hamdu Shaka alitangaza uamuzi huo jana jioni muda mfupi baada
ya Mollel kukabidhi ofisi kwa katibu mpya wa UVCCM mkoa, Saidi Goha
ambaye amehamishiwa Arusha akitokea Lindi, akiwa chini ya ulinzi wa
polisi.
Baada ya makabidhiano hayo polisi walimrejesha kituo kikuu cha
polisi anakoshikiliwa. Shaka alisema, Mollel aliandikiwa barua ya
uhamisho kwenda makao makuu tangu Agosti 25, na alitakiwa kukabidhi
ofisi ndani ya siku 14 lakini aligoma.
Alisema Mollel amekiuka kanuni za
utumishi za UVCCM, hivyo Baraza Kuu na Kamati ya Utekelezaji Taifa
watatoa uamuzi zaidi kwa mujibu wa kanuni kwa kuwa ukomo wa sekretarieti
ni kumsimamisha.
Hata hivyo, Mollel akizungumza akiwa chini ya ulinzi, alisema makabidhiano hayo ni batili kwa kuwa hakuyasaini.
Hata hivyo, Mollel akizungumza akiwa chini ya ulinzi, alisema makabidhiano hayo ni batili kwa kuwa hakuyasaini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni