Kurasa

Jumatatu, 19 Septemba 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 51 & 52 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Nikafanya kama dorecy anavyo niagiza, gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia

Endelea....
Macho yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na sehemu tulipo simama, nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, kitendo cha kukunja tu, bomu alilo lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo na kwenda kugongwa kwenye miamba na kusababisha mlipuko mkubwa na mawe yakaziba barabara kwa nyuma na kushindwa kurudi nyuma.
 
Nikafunga breki na kulisimisha gari, sote tuakashuka kwenye gari huku bastola zetu zikiwa mikononi,tukaifungua milango ya gari na kujificha nyuma ya milango kwani uzuri wake haipitishi risasi.Bastola zetu zikawa zimeelekea kwenye kona ambapo tunatarajia majambazi kutokea.Ukimya wa kama dakika tatu ukatawala, hatukuona watu ambao wanajitokeza kwenye kona, nikataka kunyanyuka
“eddy kaa chini”
 
Dorecy alizungumza kwa sauti ya ukali, nikatii kwa haraka na risasi ikapiga kwenye kioo cha gari katika mlango ambao nipo mimi.Dorecy akaanza kufyatua risasi zilizo elekea walipo majambazi, kila risasi ambayo ninaipiga mimi haikumpata mtu yoyote zaidi ya kupiga pembeni, hata kama mtu nimemlenga vizuri ila haikumpata
 
“nakosea wapi?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu
“kaza mkono”
Dorecy alizungumza, huku akiendelea kufyatua risasi kwa majambazi ambao wanatoa vilio vya maumivu kila aliye pigwa na risasi.Nikaingia ndani ya mlango na kuufunga mlango wa upande ambao nipo
“unafanya nini?”
“ngoja nikuonyeshe”
 
Nikaiwasha gari na screen(kioo), kilichopo pembeni yangu kikawaka na kuniandikia maneno yaiyo nichosha
‘system weapon empty’ ikimaanisha hakuna silaha yoyote inayoweza kufanya kazi kwani zimeisha.
“shitiii”
Nilizungumza huku nikiupiga mskani kwa kitako cha bastola
“vipi?”
“kuna, ishu nilikuwa ninaicheki kwenye hii gari.Imeisha”
“ni nini?”
“silaha, naomba hilo jaketi lako la kuzuia risasi”
 
Dorecy alinitazama kwa muda kisha akavua bullet proof yake na kunirushia upande niliopo,  nilalivaa vizuri na mara nyingi nilikuwa nikimuona mzee godwin akilivaa jinsi nilivyo livaa nikiwa mtoto mdogo.Kwani kuna siku nyumbani tulivamiwa na majambazia nyumbani, akatuvalisha sote kisha yeye alielekea kupambana nao na siri moja aliyo niambia ni kwamba jaketi hili linamionzi ambayo hata ukiwa umelengwa kupigwa risasi ya kichwa basi inaivuta na kukimbilia kifuani.
“vipi huku, mbele mimi ngoja nipande hapo juu”
 
Nilimuambia dorecy, nikapanda kwenye gemo ambalo lipo pembeni yetu, nikapanda hadi pasipo majambazi kuniona, nikatafuta sehemu nzuri ya kusimama ambayo nikawa ninawaona kwa chini, nikawahesabu kwa haraka na kuwaona wakiwa wamebaki wanne wamejibanza kwenye gari lao wakimsubiria dorecy kujitokeza, dorecy naye akawa amejibanza kwenye gari akiwasubiri wajitokeze
 
Nikaishika bastola vizuri, nikafumba jicho langu moja huku nikiitazama sehemu yenye mfuniko wa tanki la mafuta kwenye gari, nikameza mate mengi kisha nikafyatua risasi tatu mfululizo huku nikiwa nimeikaza mikono yangu, risasi mbili zikapiga pembeni, jambo lililo wachanganya jamaa.Risasi ya tatu ikapiga kwenye tanki la mafuta na kulifanya gari kulipuka, huku likinyanyuliwa juu na jamaa wote wakarushwa pembeni.Hadi gari linatua chini milango na matairi yake yalichanguka vibaya.
 
Nikashuka kwenye gemo kupitia njia niliyo pandia na kumkuta dorecy akiwa bado ameshika bastola yake akiielekezea walipo majambazi, nikatembea kwa mwendo wa tahadhari hadi ilipo gari ya majambazi, nikaanza kuhakikisha jambazi mmoja baada ya mwengine kama amekufa, ambaye ninamkuta kwenye hatua za mwisho za maisha yake nilampiga risasi ya kumsindikiza kuzimu
 
Nikageuka nyuma na kumkuta dorecy akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao, kwani haamini kama nitaweza kuwapiga risasi wezake ambao amewasaliti, nikarudi lilipo gari na kuingia, nikaliwasha hadi sehemu alipo, akafungua mlango na kuingia.Nilalipitisha pembeni gari langu taratibu kulikwepa gari linalo teketea na kuandelea na safari.Dorecy akaendelea kunielekeza njia hadi tukatokea barabara inayotokea tanga kuelekea moshi
 
“eddy, ulisha wahi kuua?” dorecy aliniuliza
“swali gani sasa hilo?”
“hapana, kwa mtu ambaye hazifanyi hizi kazi hawezi kuwa kufanya kama ulivyo fanya wewe”
“nimefanyaje?”
“ulivyo wapiga wale, risasi waliokuwa wakikaribia kufa”
“kawaida”
 
Nilimjibu huku nikendelea kuendesha gari kwa umakini, macho yangu yote yakawa ni barabarani kuangali kama polisi wa usalama barabarani wapo au hakuna.Tukaingia kwenye motel iitwayo mombo motel iliyopo kwenye barabara ya mombo
 
“una pesa?”
Nilimuuliza dorecy
“ndio”
“kachukue chakula basi”
“utakula nini?”
“bufee,nyama chukua na soda za take way”
 
Dorecy akalivua shati lake na kubaki na vest ya kiume, akaziweka vizuri nywele zake ndefu, akaichomeka bastola yake kwenye buti la jeshi, mguu wa kulia na kushuka ndani ya gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikawaona askari wa usalala barabarani, wakiingia kwenye geti la motel wakiwa na pikipiki.
Wakaisimamisha pikipiki nyuma ya gari langu na kunifanya nianze kupata wasiwasi, kwani sihitaji kumwaga damu tena katika eneo hili.Mmoja akaanza kulitazama gari langu vizuri, akaanza kulizunguka taratibu huku akilitazama kadi zake za usajili zilizo bandikwa kwenye kii cha mbele
“anataka nini huyu?”
Nilijizungumzia kimya kimya, akanionyesha ishara ya kufungua kioo cha gari langu, akanitazama kwa sekunde kadhaa
 
“habari yako afande?” nilianza kumsalimia
“salama, gari yako ilipata nini?”
“kivipi?”
“imebonyea  pembeni huku?”
“ilipata ajali, afande”
Nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukiwa umeishika bastola, huku nikiwa nimeficha pembeni ya siti yangu
“unatakiwa ukaiyooshe, kwa maana gari ya kifahari inakuwa haileti picha nzuri”
 
“sawa afande”
“insuarence yako nayo ipo katika siku za ukingoni”
“yote nitayafanya, nikifika ikulu”
Niliingiza swala la ikulu kwa maana askari, anahisi kama mimi ni miongoni mwa askari, hii nikutoka na bullet proof niliyo ivaa
“ahaaa, upo ikulu wewe?”
“yaaa”
 
“wezetu nyinyi wa ikulu muna kula kula pesa”
“tunakua pesa wapi kaka, kazi nyingi kama hizi unazo ziona”
“ila si kwa kila kazi unapata mkwanja mrefu?”
“inategemea, na kazi”
“ahaa sisi wa barabarani huku ni shida”
“shida gani?”
“ahaaa, madereva wenyewe wabishi kama nini”
“wabaneni”
 
Nilizungumza huku nikijiamini sana, kwani tayari nimesha muingiza choo cha kike huyu askari.Dorecy baada ya kuwaona askari akastuka, ila akajikaza na kwajinsi alivyo vaa askari ninaye zungumza naye akazidi kuamini kuwa sisi ni askari kutoka ikulu.
 
“habari yako, afande?”
Dorecy alimsalimia askari
“salama tuu, jamani ngoja niwaache muende”
“asante afande kwa muda wako”
“ila kaka kama kukiwa na nafasi basi, huko ikulu tukumukane”
 
“usijali kaka yangu”
“naomba namba yako ya simu”
“nitajie yako kwa maana ninabadilisha badilisha namba za simu, si unajua kazi zetu hizi”
Askari akanitajia namba yake ya simu, tukaagana naye na kuondoka bila ya wao kutustukia juu ya kitu chochote
“eddy, nimesikia ikulu?”
 
“ahaaa mzembe yule, alivyo niona nimevaa hivi akazani mimi ni askari”
Dorecy akaanza kucheka sana,
“eddy your geniuse boy”
“kwa nini?”
“umemtekaje tekaje hadi kakuamini?”
“njaa zake tuu yule, nahisi”
 
Safari ikaendela kwa mwendo wa kawaida, hadi tunafika korogwe akawa ememalia kula, nikasimamisha gari pembeni na kumpisha  dorecy upande wangu wa dereva kisha mimi nikakaa upende alio kuwepo na kuanza kula.
“eddy, tunaelekea dar au wapi?”
“dar”
“unajua mimi sio mwenyeji wa dar”
“wewe ni mtu wapi?”
 
“kagera na nimwanajeshi, ambaye nilikuwa upande wa baba yako.Alitushawishi hadi tukawa tunafanya kazi zake isitoshe yeye ni mkubwa hatukuwa na kauli juu ya hili, ndio maana ikafikia kipindi nikaamua kuwasaliti, niachane na kazi zake”
“kwani, mulikuwa munafanya kazi gani?”
“kazi nyingi tu za kigaidi, hadi kazi ile ya kukuteka wewe, mimi ndio nilikuwa muendeshaji wa gari la mbele”
“wewe ndio ulikuwa kihere here sana kwenye kunimulika mataa”
 
“ahaa  tutafanyaje sasa, wakati bosi ndio kashasema”
“na ile siku niliwapeleka”
“ahaa wee acha tuu, nilikuwa ninaendesha gari hadi mikono inaniuma”
“sasa, mulijuaje kuwa ninarudi?”
“unajua ilikuje, mzee alimpigiwa simu na askari ambao, sijui walikuwa wanakukimbiza arusha.Sasa, wale askari walikuwa wanataka kukufukuzia, ila mzee akasema wamuachie kazi yeye.Ndio maana ulistukiza gari zikiwa zinakufwata tuu”
 
“mmmmm.....”
“yaani hapa umeichokoza vita, na mzee wako anamkono mrefu sana”
“mungu bariki nitayashinda”
“yaa, kikubwa ni kupambana hadi dakika ya mwisho.Fungua hapo kuna bastola yako”
Nikafungua kwenye sehemu ya kuhifadhia vitu iliyopo mbele kwenye siti niliyo kaa, nikaikuta bastola ya mama
“niliiweka, mimi hapo”
“asante”
 
Hadi tunaingia dar es salaam, hatukupata tatizo la kusimamishwa na askari yoyote njiani, moja kwa moja tukaelekea nyumbani.Hadi tunafika nyumbani ilishatimu saa kumi na moja jioni, dorecy akasimamisha gari sehemu ya magesho ya magari baada ya geti kufunguliwa.
 
“karibu ndani”
“asante”
Tukaingia ndani na dorecy, sikumkuta mtu yoyote ndani, nikatoka na kwenda gaetini na kumuuliza mlinzi
“mama yupo wapi?”
“ni siku ya pili tangu aondoke jana na yule sister hajarudi”
“sister gani?”
“yule uliye kuja naye,majuzi”
“sheila?”
“ndio”
“powa”
 
Nikarudi ndani na kuchukua simu ya mezani na kumpigia mama simu, ikaita kwa muda kisha ikapokea
“mama upo wapi?”
“eddy.....Eddy.Umecheza pata potea”
Niliisikia sauti ya mzee godwin ikizungumza kwa dharau huku akicheka,wasiwasi ukaanza kunivaa
“yupo wapi mama yangu?”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali
 
“mama yako ame reast in peace”(.......Amepumzika kwa amani)
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, huku jasho jingi likimwagika midhili ya maji, dorecy akasimama kwenye sofa na kunifwata sehemu nilipo, akanipokonya simu na kuishika mkononi
“haloo.....Eddy........Ulisema ufe wewe, kwa ajili ya mama yako.Ila kwa bahati mbaya mama yako ndio hivyo amesha tangulia mbele za haki”
 
Sauti ya mzee godwin iliendelea kusikika kwenye simu akizungumza kwa sauti iliyo jaa dharau
“do you know, who will be the next to die?”(je una unajua, ni nani atafwata kufa?)
“hhahaahaaaa is your sheila, na leo nimepata tunda lake kwa mara nyingine tena, yupo so mwaaaaaaaaaa”(hhahaahaaaa ni sheila wako, ........)
 
“enjoy  your day, mr eddy”(furahia siku yako, bwana eddy)
Simu ikakatwa, nikashindwa kuyazuia machozi yangu, kwa mara nyingine mzee godwin anawateka watu wangu wa karibu.Dorecy akanishika mkono na kunikalisha kwenye sofa, hasira taratibu ikaanza kupanda na kujikuta mwili wangu wote, ukianza kunitete, dorecy akanitazama kwenye macho yangu.Mlango wa kuingilia ndani ukafunguliwa na kujikuta nikichomoa bastola yangu na kumuelekezea mlinzi aliye fungua mlango
 
“ohooo, ni mimi kaka”
Alizungumza huku akiinyanyua mikono yake juu, huku mkononi akiwa ameshika gazeti
“unataka nini?”
Nilimuuliza kwa sauti ya ukali
“ka..Ka kuna hili gazeti hapa.....”
“la nini?”
“kukuuu.....”
 
“nitolee kigugumizi chako, kabla sijakuua”
Mlinzi akaanza kutoka ndani
“wee kaka samahni, hembu hilo gazeti”
Dorecy akanyanyuka na kwenda kulichukua gazeti, akalifungua na kuanza kulisoma huku akipiga hatua za taratibu akirudi sehemu ambayo alikuwa amekaa.Akakaa sehemu yake, sikuwa na haja ya kulitazama gazeti lake.
“eddy”
 
Dorecy aliniita na kunifanya nimtazame, nikaikuta sura yake ikiwa imejaa mikunjano akionekana kuna habari iliyopelekea sura yake kuwa katika sura kama hii,akanyanyuka na kukaa kwenye sofa nililopo mimi.
“soma, hii habari”
Macho yangu yakatua kwenye maandishi meusi yaliyo andikwa kwa herufi kubwa zinazo onekana vizuri pasipo na shida yoyote
 
‘mtoto wa waziri wa afya (eddy godwin), anatafutwa na jeshi la polisi kwa mauaji ya kikatili ya mfanya biashara wa madini jijini arusha bwana derick lambart na mwili wa derick kuwa chakula cha mbwa wake’
Chini ya maandishi haya makubwa kuna picha yangu, ya mama na derick lambart zikiwa zimeambataishwa kwenye mstari mmoja
“eddy ni kweli?”
 
Dorecy alizungumza huku akinitazama machoni, sikumjibu zaidi ya kunyanyuka kwenye sofa, kabla sijamjibu dorecy nikasikia mlio wa gari ukisimama nje ya geti.Cha kwanza nikazima taa za sebleni na kufungua pazia kidogo la dirisha linalo tazama kwenye geti,nikawaona askari wawili wakizungumza na mlinzi huku wakionekana kulazimisha kuingia ndani kwa nguvu..................................
Endelea na sehemu ya 52 kupitia ubuyublog.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni