Wilbrod Frank Lukamilwa
Mtanzania Wilbrod Frank Lukamilwa
alitiwa mbaroni siku ya Jumanne iliyopita Septemba 6, 2016 baada ya
polisi wa kaunti ya Montgomery jimbo la Maryland kumtafuta zaidi ya
mwaka bila mafanikio huku polisi ikiwa imetoa $10,000 kwa yeyote
atayetoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwake.
Wilbrod Frank Lukamilwa miaka 41, mkazi
wa Takoma, Jimbo la Maryland siku hiyo ya Jumanne Polisi wa kauti ya
Montgomery wakiwa mjini Silver Spring wakigawa vipeperushi vyenye picha
yake kwa wapita njia, ndipo mtu waliyekua wakimtafuta zaidi ya mwaka
alipopita mbele yao na yeye bado kidogo polisi hao wangemgawiya
kipeperushi hicho.
Mmoja wa Polisi hao aliweza kumtambua
kwa kumfananisha kwenye picha iliyokua kwenye kipeperushi na kumwita
jina na yeye alipogeuka na Polisi kumkamata kirahisi.
Wilbrod Fank Lukamilwa ameshtajiwa na
mtu mmoja ambaye anadai alimlipa pesa kwa ajili ya mafunzo ya awali ya
chuo cha unesi baada ya Lukamilwa kujitambulisha kwake kuwa yeye ni mkuu
wa chuo cha unesi cha hospitali na angeweza kumsaidia mtu huyo kujiunga
na masomo ya unesi katika hospitali hiyo.
Mtu huyo inadaiwa kukutana na Lukamilwa
mwaka 2012 na tangia mwaka 2015 polisi wamekua wakimtafuta Wlbrod Frank
Lukamilwa bila mafanikio.
Chanzo: zanzibarnikwetu.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni