Jumatano ya Septemba 14 2016 chama cha soka barani Ulaya UEFA kimefanikiwa kumpata Rais mpya wa chama hicho ambaye atamrithi Michel Platini katika nafasi hiyo, UEFA imefanikiwa kumchagua Aleksander Ceferin kuwa Rais wao mpya.
Ceferin ambaye alikuwa Rais wa chama cha soka cha kwao Slovenia toka 2011, amechaguliwa leo na kutangazwa, baada ya kuungwa mkono na vyama 42 kati ya 55 vya soka barani Ulaya, Ceferin sasa anachukua nafasi hiyo iliyokuwa inakaimiwa na Angel Maria Villar kama Rais toka October 2015 baada ya Platini kuwa katika tuhuma za rushwa.
Aleksander Ceferin mwenye umri wa miaka 48 ni mtaalam wa masuala ya sheria na amefanikiwa kumshinda mpinzani wake Michael van Praag mwenye umri wa miaka 68, Ceferin anaingia kuchukua nafasi hiyo na atadumu nayo hadi 2019 ambapo Platini ndio alikuwa anamaliza muda wake kabla ya kufungiwa miaka minne na FIFA kujihusisha na soka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni