Gharama za maisha zinazidi kupanda
kila siku katika miji mbalimbali duniani, shirika la Mencer
limeziorodhesha gharama za bidhaa na huduma 200, pamoja na malazi,
huduma za chakula, starehe, usafiri wa umma na huduma za kijamii na
kupata orodha ya miji inayoongoza kwa gharama zaidi za kujiendesha
kimaisha.
Hii ni list ya miji kumi iliyotajwa kuongoza kuwa ghali zaidi kuishi barani Afrika.
10-ABUJA
Mji mkuu wa Nigeria na wenye mpangilio
mzuri pamoja na wakazi zaidi ya 979,876 na ulianza kujengwa kwenye
miaka ya 80, ukiongelea Abuja Rais wa kwanza wa Afrika Kusini alishawahi
kujisemea …”kwanini tuende ulaya wakati tunayo ulaya hapahapa”
akimaanisha maisha ya Abuja hayatofautiani na nch za ulaya kutokana na
gharama kubwa za maisha.
9- Conakry ni mji wa kibiashara na
mkubwa zaidi nchini Guinea unatajwa kuwa kati ya miji ya gharama zaidi
kuishi katika bara la Afrika, kwa bahati mbaya licha ya mji huu kuwa mji
wa gharama bado miundombinu yake sio mizuri katika baadhi ya maeneo.
8-Bamako ni mji mkuu wa Mali na moja
kati ya miji ya gharama Afrika makampuni mengi ya kigeni na mashirika ya
misaada yameweka makazi yao katika mji huo. Watu hawa huhitaji kuishi
kama nchi za ulaya hii imeongeza gharama za kimaisha mjini humo.
7- Brazaville ni mji mkuu wa Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na matajiri ama watu wenye pesa ndio wenye uwezo
wa kukabiliana na gharama za maisha kutokana na bei za matumizi kuwa
juu kulinganisha na miji mingine ya Afrika.
6- Lagos ni mji mkubwa wa kibiashara
nchini Nigeria na matajiri wengi wanaishi katika visiwa vya jiji hilo,
foleni za magari ni kitu cha kawaida katika mji huu wa gharama barani
Afrika.
5- Kinshasa, mji huu una zaidi ya watu
millioni 4 ikiwa ni mji mkubwa wa kibiashara nchini Congo sifa zake ni
pamoja na usalama wa uhakika kwa wageni.
4- LIBREVILLE ni mji mkuu wa
Gabon unaotajwa kuwa na wakazi zaidi ya laki tano, Gabon ni moja kati
ya nchi zenye utajiri wa maliasili pia inapokea misaada mingi kutoka
kwenye nchi zilizoendelea. Mji huu unasifika kwa kuwa na kumbi za
starehe (klabu) za gharama kubwa.
3- VICTORIA ni mji mkuu wa Shelisheli
umetajwa kuwa kati ya miji ya gharama kubwa kuishi Afrika , alishawahi
kufika Prince William wa Uingereza na mke wake wakati wa Honeymoon na
iliripotiwa kwamba kwa usiku mmoja walilipia chumba kwa dola 5,000 jinsi
gani ambavyo hotels na nyumba za ufukwe huo ni ghali.
2- N’Djamena ni mji mkuu wa Chad, ingawa
umetajwa kuwa mji wa pili ambao ni ghali zaidi kuishi barani Afrika,
hauna miundombinu ya kutosha, hakuna reli wala bandari katika mji huu.
1- LUANDA, mji mkuu wa Angola na pia mji
ghali zaidi kuishi kuliko yote barani Afrika na pia upo katika list ya
miji ghali zaidi kuishi duniani mji huu kupanga nyumba kwa euro 10,000
mpaka euro 30,000 ni kitu cha kawaida kwenye mji huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni