Kurasa

Jumamosi, 17 Septemba 2016

Serikali ya Zimbabwe Yatoa Onyo Kali kwa Watakaofanya Maandamano

 Maandamano yameshuhudiwa nchini Zimbabwe miezi ya hivi majuzi

Serikali ya Zimbabwe imewaonya waandamanaji ikiwataka wazishiriki maandamano kwenye mji mkuu Harare.

Waziri wa mambo ya ndani alisema kuwa vikosi vya usalama vitalinda kwa ukamilfu kile alichokitaja kuwa amani.

Polisi wametoa onyo wakisema kuwa wale watakaokamatwa kwa kushiriki maandamano hayo watafungwa hadi mwaka mmoja.
Rais Robert Mugabe ana umri wa miaka 92

Kumekuwa na maandamano ya kila mara miezi ya hivi karibuni yanayotaka kufanywa mabadiliko katika upigaji kura na kuondolea madarakani kwa Rais Robert Mugabe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni