Kurasa

Jumamosi, 17 Septemba 2016

Kanye West afunguka asema nikifa ndio mtaelewa umuhimu wangu kwenye fashion

Rapper Kanye West anaamini kuwa bado watu wanamchukulia poa kwenye biashara yake ya fashion na kwamba anaamini siku akifa ndio wataelewa.

Amesema hayo kwenye mahojiano na jarida la W.

“Sidhani kama kuna yeyote kwenye upande wangu,” alisema Kanye. “Hadi leo hawaelewi mimi nani. Hawataelewa hadi nitakapokufa. Naeleweka vibaya na hakuna mtu kwenye fashion aliyepo upande wangu,” alilalama.

Anadai kuwa watu kwenye fashion hawajui ujuzi wake na anadhani hawajui anachokifanya. Uzinduzi wa Yeezy Season 4 mwezi huu ulikoselewa vikali na wataalam wa mitindo, wakidai kuwa hajali anapowatumia wanamitindo wachanga.

“Watu wachache sana hata wanajua kuwa mimi nina Ph.D. kwenye sanaa,” alisema.

Hata hivyo amesema licha ya kuchukuliwa poa anaamini mafanikio ni zaidi ya kuingiza fedha bali kufanya kitu chenye faida kwa wengi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni