Baada ya kuonekana kuanza kuwa na afya njema baada ya kupambana
kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, Ray C ameonekana kuanza
kuingia studio kurekodi wimbo wake mpya.
Kupitia mtandao wake wa Instagram, muimbaji huyo ameandika mashairi ya wimbo wake huo mpya ambao ameupa jina la Panya Road.
Haya ni mashairi yake:
Verse 1:
Hivi ukimkamata panya road wako anaekugombanisha anaekugombanisha na marafiki zako
Kupeleka fuko la umbea mpaka kwa mume wako
Ashakugombanisha na majirani mtaa mzima,
Panyaroad asilielipa hata senti
Lakini kapangisha bureeee kichwani mwako
Yani mpaka akitokea mtaani kwako kama ulikaa kibarazani lazma utoke mbio Kama umewaona alshabab!!!!!
Maana huyo hata salaam tu ukimpa tafrani
Kama kuna MTU kakuona umesimama naye japo dakika akitoka hapo
Huyo panyaroad akikutana na yule aliewaona mko wote utajuta
Kwanini ulimpa salam yako
Maneno atakavyobadilisha na kutia chumvi na ndimu
Mamaa mbona kigodoro cha michambo utaamka nacho mlangoni mwako
Hata mapanga ya hao panyaroad yana afadhali????
Haya ndo mbea wenu mshamjua na mshamweka kati mtaa mzima!kinachofata??????
Baada ya kuandika verse hiyo ya kwanza, Ray C ameandika kwenye mtandao
huo ujumbe unaosomeka, “aaaaaaah hebu subirini msije rusha ngumu
haitaingia studio mi nataka maneno ya michambo tu niongezee kwenye verse
ya. Pili .”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni