Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika
wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao
chakula cha mchana.
JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa
muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao
mambo mbalimbali kuhusu muziki wao.
Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais
huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu
muziki.
“Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma
Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam
aliandika instagram.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni