Cristiano Ronaldo amemchana makavu ‘Laivu’, Xavi Hernandez baada ya
mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kusema Mreno huyo anayetisha Real
Madrid hana bahati kutokana na kuishi zama hizi za Lionel Messi.
Kauli hiyo inamaanisha nyota wa Argentina, Messi, ndiye mchezaji bora wa muda wote na uwepo wake unamnyima hadhi hiyo Ronaldo.
Hata hivyo, Ronaldo, amejibu mapigo muda mfupi baada ya kuisaidia timu
yake kushinda mabao 5-2 dhidi ya Osasuna ikiwa amerejea kutoka kwenye
majeraha.
‘Mchezaji wanayemperuzi zaidi kwenye Internet ni mimi’. Amesema Ronaldo.
‘Wote wanaotaka kuuza kurasa za mbele (kwenye magazeti) au wanaotaka
kutangaza vitu vyao, wananizungumzia mimi’.
‘Alichosema Xavi kina faida gani kwangu? Anacheza wapi? Huko Qatar au
(kwingine), sijui. Alishinda kila kitu, lakini hajawahi kushinda Ballon
d’Or. Mimi ninazo tatu’
Kwa upande wa Messi ameshinda Ballon d’Ors tano na anachukuliwa kuwa
mchezaji bora wa muda wote, lakini Ronaldo anaamini kwamba yeye
anastahili hadhi hiyo.
Baada ya kuichezea Barcelona kwa miaka 18, Xavi alitimkia Al Sadd ya Qatar ambako anamalizia maisha yake ya soka.
Akizungumza na Redio ya Hispania ya Cadena Ser mapema wiki hii, Xavi
alisema: ‘Ni mpumbavu tu ambaye amecheza soka na asitambue kuwa
Cristiano ni mcheza mpira wa kiwango cha juu. Lakini ana bahati mbaya
kuishi katika zama hizi za Leo”.
Mwanasoka bora wa Ulaya, Cristiano Ronaldo (kulia) akishangilia na
mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Gareth Bale baada ya kufunga katika
ushindi wa 5-2 dhidi ya Osasuna kwenye mchezo wa La Liga Uwanja wa
Bernabeu.
Mabao ya Real yalifungwa na Ronaldo dakika ya sita, Danilo dakika ya 41,
Ramos dakika ya 45, Pepe dakika ya 56 na Modric dakika ya 62, wakati ya
Osasuna yalifungwa na Riera dakika ya 64 na David Garcia dakika ya 78.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni