Kurasa

Jumatatu, 12 Septemba 2016

Hillary Clinton augua ugonjwa wa homa ya mapafu katika kumbukumbu ya wahanga

Bi Clinton akisaidiwa kuingia katika gariBi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari 

Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amegundulika kuwa na ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa.

Akijerea baada ya kupata nafuuAkijerea baada ya kupata nafuu 
Amesema pia Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Clinton aliondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.

Donald Trump alihudhuria hafla hiyoDonald Trump alihudhuria hafla hiyo 
Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.
Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.
Chanzo bbcswahili.com
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni