Ikiwa mtawala au Omukama kama anavyojulikana lugha yao akifuatiwa na ukame, nzige, majanga ya magonjwa huchukuliwa kama kiongozi mwenye mkosi au balaa kwa watu wake na enzi hizo walikuwa wanatambikia (okutelekelela) ili kuomba mizimu kupunguza ipunguze mbinyo baada ya kumchukia mtawala.
Kinyume chake ni mtawala (Omukama) anayekuja na mvua hufuatiwa na chakula tele (Omwelo) na watu hufurahi na kumuona mtawala aliyekuja na baraka. Mkapa angekuwa anaishi Kagera angepata shida sana baada ya ajari ya Mv Bukoba. Zilitungwa nyimbo na za kimila kulaani ajari (MV Bukoba ekitaliwa igamba).
Baada ya tetemeko la jana kutafuatiwa na imani za wanakagera kuchukua nafasi yake. Wanasema haijawahi kitokea tetemeko la namna ile katika historia ya mkoa huo. Watu wamekufa, majengo yameporomoka, barabara zimepasuka, majeruhi ni wengi. Imetonesha majanga ya Mv Bukoba, na ugonjwa wa Ukimwi vilivyourudisha nyuma mkoa huo kwa kiasi kikubwa. Swali ni je itamuunganisha 'mkulu' anayechukuliwa kama mwenyeji wa mkoa huo kwani Chato ilitengwa toka mkoa wa Kagera.
By mpk
![]() |
Add caption |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni