Kurasa

Jumanne, 20 Septemba 2016

Ajabu: mtoto wa Bungoma Kenya anayezungumza kama mtu mzima!

Mtoto msichana wa miezi mitatu anaitisha chakula vizuri napohisi njaa.

 Mtoto wa miezi mitatu awashtua wakazi wa Bungoma kwa kuzungumza kama mtu mzima

– Mtoto huyo msichana kwa jina Joy Wangila anaomba chakula na kuzungumza na majirani vizuri kabisa

Wakazi wa kijiji kimoja katika eneo la Magharibi mwa Kenya wameachwa vinywa wazi baada ya mtoto mchanga kuzungumza kama mtu mzima.

Wakazi katika kijiji cha Bilaa B kwenye eneo bunge la Tongaren, Kaunti ya Bungoma, walishangaa kumsikia mtoto huyo msichana kwa jina Joy Wangila akiomba chakula na kuzungumza na majirani vizuri.
 Mtoto wa miezi mitatu amewashangaza wakazi wa Bungoma kwa kuzungumza vizuri kabisa kama mtu mzima.

Ni kisa ambacho kimefanya kijiji hicho kuwa maarufu kwani kimefurika wageni kutoka sehemu mbalimbali wanaotaka kushuhudia moja kwa moja maajabu hayo.
Familia ilipigwa na butwaa kumsikia mtoto huyo mchanga akizungumza, na sasa wamekuwa kivutio kijijini kwani watu wanafurika nyumbani kwao kushuhudia maajabu hayo.
Wazazi wa mtoto huyo, Patrick Wasike na Salome Wangila, sasa wanawataka wazee wa jamii hiyo ya Bungoma kumfanyia mwana wao uchunguzi kubaini kinachojiri kwani ni jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa hapo.

“Mwanangu anatamka maneno …akitaka chakula anaomba vizuri kabisa. Ukikataa kumpatia anaangua kilio,” Mama Salome alisema kumhusu mwanawe.

Nyanyake mtoto huyo alisema kuwa alianza kuzungumza Agosti 2, 2016.

“Mamake alitaka kumnyonyesha lakini mtoto alitaka uji.

 “Nikamsikia tena akizungumza nilipokuwa nikichimbua viazi ili kuvitayarisha kwa chakula cha mchana. Jirani alikuja kuomba viazi hivyo na mtoto huyo akamuambia asithubutu kuja nyumbani hapa kula chakula chochote,” alieleza kutoka kijiji hicho cha Bilaa B mjini Bungoma.

chanzo:Mungwana blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni