Kurasa

Ijumaa, 23 Septemba 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 55 & 56 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA....
 “Sali sala yako ya mwisho?”
Dorecy alizungumza huku sura yake ikiwa imejaa jasho jingi, na mikonjo iliyonifanya niamini huu ni mwisho wa maisha yangu mimi Eddy Godwin

ENDELEA....
“Dorecy umechanganyikiwa?”
Nilimuuliza Dorecy anayeonekana kumaanisha kile kitu anacho kizungumza, hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuendelea kunielekezea bastola yake kwenye sura yangu
“Eddy usimuamini kila unaye muona utaumia sawa?”

Dorecy alizungumza na gafla nikastukia akinipiga na kitako cha bastola kwenye kichwa changu, giza lililo andamana na maruwe ruwe kitanitawala taratibu katika macho changu na kwa mbali nikausikia mlango ukifunguliwa, baada ya muda kidogo sikujua ni kitu gani kinacho endelea  

Nikahisi nikiguswa mgongoni, taratibu nikayafumbua macho yangu na kukutana na viatu vya mwanaume vikiwa vimesimama kando yangu, nikakinyanyua kichwa changu  taratibu huku nikiwa ninamaumivu makali, nikakutana na sura ya mwanaume ambaye amevalia sare za wahudumu wa hoteli hii

“Kaka, habari yako”
Jamaa alinisalimia, huku akinitazama usoni mwangu.Sikumjibu cha kwanza kutazama ni kuangalia sehemu nilipo weka begi langu lenye madini ndani, sikuliona na kujikuta nikikurupuka na kusimama, nikaingia bafuni na kukuta kweupe hakuna mtu

“Kaka vipi?”
“Ku..kunaa dada hiv...i mrefu ume...muona wapi?”
“Yule uliye ingia naye jana usiku?”
“Jana, usiku? Eheee huyo huyo”
Niliungumza huku nikipiga hatua kuelekea kwenye dirisha, nikatamani kuanguka chini na kupoteza fahamu, kwani mwanga mkali wa jua nilio ukuta nje ya dirisha umenichanganya kiasi kwamba nimekosa la kuzungumza

“Yule mbona aliondoka usiku ule ule?”
“Shitii”
“Kwani, hamujuani?”
“Ehee”
“Hamujuani?”
Hata sikujua nimjibu vipi, muhudumu huyu aliye simama mbele yangu, nikajichunguza na kugundua kuna damu zilizo mwagika kwenye shati langu la kiaskari nililo livaa.
“Unamichirizi ya damu puani kaka”

Muhudumu alinionyesha, nikasimama kwenye kioo kilichopo kwenye hichi chumba na kujikuta ni kweli nilitokwa na damu za puani, ambayo kwa sasa imekauka.Muhudumu akanipatia  taulo na nikaanza kujifuta
“Alafu, kuna askari walinionyesha picha yako mida ya asubuhi, na kuniuliza kama wewe upo kwenye hii hoteli nikwaambia kwamba uliondoka jana usiku”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, huku wasiwasi mwingi ukianza kunitawala

“Waliondoka?’
“Ndio waliondoka, ila sijajua kama watarudi tena au la”
“Asante ndugu yangu”
Nikatizama chini, na sikuona bastola zangu nikatambua ni lazima Dorecy atakuwa ameondoka nazo zote,
“Kaka kwani wewe ni askari kweli?”
Jamaa aliniuliza, nikamtazama kuanzia juu hadi chini, kwani maneno ya Dorecy aliyo niambia nisimuamini mtu yakaanza kunirejea kichwani mwangu
“Kwani vipi?”
“Nimeuliza hivyo kwa nia nzuri tu?”
“Nia gani?”

“Kwa maana picha ya sura yako, sio mara yangu ya kwanza kuiona kwenye mach yangu”
“Ulisha wahi kuiona wapi?”
“Wewe si ndio, Eddy?”
Sikustushwa sana kwa maana ninatambua kwamba ninatafutwa karibia nchi nzima ya Tanzania kwa tukio la kumuu Derick
“Mimi sio Eddy?”
“Sawa”

Nikatoka nje ya chumba, nikatizama kwenye kordo zote na kuona hakuna dalili ya kuwa na mtu, nikaanza kutembea kwa hatua za haraka kuelekea kwenye ngazi za kushuka chini, nikaanza kushuka kwenye ngazi ya kwanza, nikaisikia miguu ya watu wakikimbia na kunilazimu kuchungulia chini, nikaona kundi la askari wapatao sita wakipandisha ngazi kwa haraka huku wanne wakiwa na bastola na nyuma yao wakiwa wameongozana na mzee mwenye kitambi kwa haraka nikatambua ni meneja wa hii hoteli.Nikarudi juu haraka na kukutana na muhudumu niliyekuwa chumbani
“Tupandishe huku juu”

Aliniambia huku akitangulia kupandisha ngazi za kuelekea ghorofa ya juu, tukapandisha ghorofa ya juu na kutokea kwenye moja ya mlango wenye ngazi za chuma zilizo elekea chini.Tukaanza kushuka kwa haraka
“Huku ni nyuma ya holet”
Aliniambia, tukashuka hadi chini, tukakuta kijimlango kidogo, kilichopo kwenye ukuta na tuapita na kutokea kwenye hoteli nyingine niliyokuta kibao kikubwa kilicho andikwa ‘Macarios Hotel’

“Tupite huku”
Tukakatiza kwenye reli, na kushika barabara ya kuelekea magharibi kwetu na kutukea kwenye barabara moja inayopitisha magari mengi
“Hapa kunaitwa kwaminchi”
“Sawa”
Tukaendelea kukatiza mitaa, na kufika kwenye mtaa mmoja ulio na nyumba nyingi zilizo banana sana

“Hapa ni mwamboni”
“Kupo kama mbagala”
“Kwa nini?”
“Nyumba zake jinsi zilivyo”
“Karibu ndani”
Tukaingia kwenye nyumba iliyo chakaa kiasi fulani, akanikaribisha ndani kwake, ambapo kuna kitanda na kistuli kimoja, pamoja na nguo baadhi
“Karibu kaka”
“Asante”

Nikakaa kwenye kiti na yeye akaketi kwenye kitanda chake
“Kwa jina mimi ninaitwa Mbasa, ni mwenyeji wa bara, mkoa wa Shinyanga huko”
“Ahaaaa, kwanza ninashukuru kukufahamu, pili ninashukuru kwa kunisaidia”
“Kusaidiana ni jamba la kawaida, hususani kwa vijana kama sisi ambao tunatakiwa kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha tunafikia kwenye malengo yetu”
“Nikuulize kitu Mbasa?”
“Uliza tuu”

Unawezaje kumsaidia mtu usiye mjua?”
“Kaka Eddy, mimi ninakujua na nimekuwa nikifwatilia habari zako kwenye magazeti jinsi unavyo tafutwa na jeshi la polisi kwa mauaji ya bwana Derick”
Nikamtazama jamaa vizuri, nikajitazama na mimi vizuri nikajisemea kimoyo moyo hata akitaka kuanzisha ugomvi, ninamudu tena sana
“Isitoshe, nilivutiwa sana na wewe”

“Kwa nini?”
“Umri wako na matukio yako uliyo yafanya ni tofauti”
“Sawa, ila ninakuomba usimuambie mtu juu ya uwepo wangu hapa kwako”
“Si wezi kwa maana ninahitaji tusaidiane”
“Tusaidiane?”
“Ndio, shida uliyo kuwa nayo wewe kidogo inaendana na yakwangu?”
“Shida gani”

“Nilizaliwa kwenye familia ya maisha bora, baba alikuwa anamiliki migodi ya madini, alikuwa ni tajiri sana.Ila niliaziliwa peke yangu kwa bahati mbaya mama yangu alifariki kwa ajali ya gari, nilikuwa darasa la sita”

“Baba alilazimika kumuona mwanamke mwengine, ambaye alikuwa ni binti mdogo kiasi na alijaliwa uzuri halisi kutoka kwa Mungu, kutokana na kazi nyingi za baba tangu, alitumia muda mwingi sana kuwa mbali na mama mdogo, ikafikia kipindi nikawa na mahusiano na mama mdogo”

“Badi mama mdogo alipata ujauzito wangu na mbaya zaidi niliwahi kubalehe haraka sana, ule ujauzito tuliulea katika mzingira ya kificho na ninacho mshukuru MUNGU, baba alisafiri kikazi kwenye Ujerumani na alikaa mwaka na nusu so ile ishu hakuijua”
“Mwanangu alizidi kukua pasipo baba kujua hilo, hadi anatimiza miaka mitatu, kama unavyo jua dunia haina siri baba yangu akaja kuligundua lile swala la mimi kuzaa na mama mdogo”

“Huwezi kuamini, kuna siku baba alituomba twende naye shambani, hatukuwa na kipingamizi kutokana tulikuwa hatujui kinacho endelea”
“Ngoja kwanza hapo mtoto wenu mulikuwa mumemuweka wapi?”
“Mtoto, tulimpeleka kwa dada yake yule mama mdogo, pesa za matumizi mimi ndio nilikuwa ninazipeleka pasipo baba kuelewa mchezo”

“Sasa tuifika shambani, tukiwa na mama mdogo, pamoja na baba.Tulikuta watu wake ambao mara chache huwa ninawaona ona, huwezi amini nilimkuta mwangu akiwa ametundikwa juu ya mti huku ngozi yake ikiwa imechunwa kama mbuzi aliye chunwa ngozi”

“Baba, yangu alitugeukia hapo hapo na kuanza kumshambulia mama mdogo kwa ngumi na mateke, huwezi ukaamini nilimshuhudia mama mdogo akichemshwa katika pipa lenye mafuta ya kula, huku akiwa hai, cha kumshukuru MUNGU, niliweza kufanikiwa kukimbia ila niligwa risasi za ya paja na kuanzia hapo sikuweza kumuona baba tena kwenye maisha yangu”

“Ila nilikuja kugundua kwamba baba pia alihusika na ajali ya mama”
“Kisa kilikuwa ni nini?”
“Hadi leo sijajua kisa kilikuwa ni nini hadi baba akaamua kumuua mama”
Nilimsikiliza Mbasa vizuri sana, kidogo yeye ana nafuu sana katika simu lizi ya maisha yake ya nyuma

“Baba yako anaitwa nani?”
“Godwin?”
Nikastuka, na kumtazama vizuri
“Mbona unastuka kaka Eddy?”
“Anaitwa Godwin, yupoje poje?”
“Mrefu kiasi, ni maji ya kunde kidogo, anamwili ulio jazia kidogo na pia anakovu kwenye mkono wake wa kulia, mama aliniambia baba alipataga ajali akiwa kijana”

Sifa ambazo Mbasa alinielezea zifanana na sifa za Mzee Godwin ambaye hapo mwanzo niliamini ni baba yangu ila ukweli ni kwamba ni baba yangu mkuwa, ila kitu kinacho nichanganya ni Mzee Godwin ninaye mjua mimi ni Mwanajeshi

“Ana kazi nyingine anayo ifanya ukiachilia na madini?”
“Ndio, nilikuja kushangaa siku nilipo sikia kwamba amepewa cheo cha kuwa mkuu wa jeshi wakati sijui hata jeshi yeye amekwenda lini?”
Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, nikamtazama Mbasa kuanzia juu hadi chini na kujikuta nikitingisha kichwa kwa kumuonea huruma

“Vita iliyupo mbele yetu ni kubwa sana”
“Kivipi?”
“Mbasa kwanza una umri gani?”
“Miaka ishirini”
Nikatabasamu, tabasamu lililo jaa uchungu kwa kumuonea huruma
“Adui yako ndio adui yangu”
Nilimuambia Mbasa na kumfanya abaki amenitumbulia mimacho.....
Endelea nayo sehemu ya 56 kupitia ubuyublog.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni