Hivyo nimekuletea njia natural ya kuondoa weusi huo bila kutumia madawa makali.
1.TUMIA MAFUTA YA NAZI NA NDIMU.
Fata step hizi::
- Chukua vijiko 3 vya mafuta ya nazi changanya na ndimu nusu
- Paka sehemu yenye weusi katika mapaja huku ukisugua kama unafanya massage kwa dakika 15.
- Kisha osha na maji ya uvuguvugu na kausha kwa kitambaa kilaini na kisafi.
2.TUMIA MCHANGANYIKO WA SUKARI ASALI NA NDIMU.
Mchanganyiko huu pia unaweza ukaondoa weusi katika mapaja na makwapa, fuata step hizi::
- Changanya kijiko kimoja cha asali, ndimu nusu na kijiko kimoja cha sukari.
- Paka sehemu yenye weusi na sugua kawaida hadi sukari ipotee.
- Acha ikae kama dakika 10 kisha osha na maji ya uvuguvugu.
3.GANDA LA CHUNGWA NA ASALI
Fuata step hizi::
- Chukua ganda la chungwa na kijiko kimoja cha asali.
- Kamua hilo ganda maji yake yangie kwenye asali.
- Kausha nakusaga hilo ganda kisha poda yake ichanganye na asali
- Paka mchanganyiko huo katika sehemu yenye weusi, kaa kwa muda wa dakika 15
- Osha na maji ya kawaida hadi kugandaganda kupotee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni