Serikali imezifnga kwa muda usiojulikana shule za bweni za wavulana za
Ihungo na Nyakato zilizoko mkoani Kagera ambazo miundombinu yake
iliathirika sana kutokana na tetemeko la ardhi liliyoyakumba maeneo
mbalimbali yaliyoko mkoani humo na kusababisha hasara kubwa.
Agizo la kuzifunga shule hizo limetolewa na waziri wa sera, bunge, kazi,
vijana, ajira na walemavu, Jenista Mhagama, baada ya kutembelea shule
hizo na kujionea hali mbaya ya miundombinu iliharibiwa vibaya na
tetemeko ambayo ni pamoja na madarasa, mabweni na vyoo hali iliyokuwa
ikiwalazimu wanafunzi kulala kwenye viwanja.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa taifa wa chama cha NCCR -mageuzi James
Mbatia ameonyesha kutoridhishwa na hatua ambazo serikali imeishazichukua
kwa waathirika wa tetemeko hilo, nao baadhi ya waathirika wa tetemeko
wameanza kupokea misaada toka wahisani miongoni mwa waathirika ni
Winfrida Paul ambaye amepokea msaada ulitolewa na chama cha walimu (CWT)
Bukoba mjini na Saad Yusuph mlezi wa kituo cha kulea watoto cha Uyacho
aliyepokea msaada toka kwa mbunge wa viti maalumu Bukoba Savelina
Mwijage ambao wanaeleza changamoto walizonazo kwa sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni