Huenda sumu ya adhabu ya BASATA kwa Nay wa Mitego ikawa haikukolea vyema.
Ni sababu rapper huyo ameibuka na kudai kuwa, hakuna mtu anayeweza
kumpangia aina ya muziki wa kufanya, na kwamba hivi karibuni ataachia
wimbo uitwao ‘Utakula Jeuri Yako’ ambao ni makavu kwa kwenda mbele na
huenda ukazua ‘sheshe’ jingine.
“Nobody can stop me,” alisema Nay katika mahojiano kipindi cha Extra
Fleva, cha Uplands FM ya Njombe kinachoendeshwa na Ergon Elly. “Muziki
wangu uko pale pale, kitu ninachowaahidi mashabiki wangu, soon, siku
nikiamka tu kuna wimbo unaitwa ‘Utakula Jeuri Yako’ patawaka.”
Nay alisisitiza kuwa hata katiba hairuhusu mtu kumzuia mtu mwingine kitu cha kuongea.
Hivi karibuni Nay alifungiwa kwa ufupi kujihusisha na muziki na kupigwa
faini ya shilingi milioni 1 kutokana na maudhui ya wimbo wake Pale Kati
uliofungiwa.
Alisema kuwa adhabu hiyo ilikuwa na madhara kiasi kwa muziki na biashara yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni