Kurasa

Jumapili, 11 Septemba 2016

Tume ya Mufti inaanza kazi rasmi ya kufuatilia mali zote za BAKWATA

Tume ya Mufti wa Baraza kuu la waislam Tanzania- Bakwata ya kuchunguza na kubainisha mali,mikataba isiyofaa na rasilimali za baraza hilo ya watu wanane iliyoundwa na Mufti hivi karibuni inaanza kazi rasmi ya kufuatilia mali zote za bakwata zilizouzwa na kuingia mikataba ili hatua stahiki zichukuliwe kuzirejesha mali hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Makamu M/kiti wa Tume hiyo Sheikh Issa Othman Issa ametaja baadhi ya hadidu za rejea za tume hiyo itakayofanya kazi kwa siku 90 ni pamoja na kufuatilia mikataba yote ya Uuzwaji wa mali za bakwata ikiwemo Viwanja,nyumba za waqfu nchi nzima,pamoja na mikataba mbali mbali ya Ubia.

Aidha Tume hiyo imewataka waislam nchini pamoja na wananchi mbali mbali kushirikiana kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kubaini mali zote za bakwata nchi nzima ambazo zimeuzwa ama kubadilishwa umiliki kinyemele ili zirejeshwe chini ya baraza kuu huku wahusika wote waliousika katika udanganyifu huo kufikishwa ktik vyombo vya sheria.

Katika salam zake za Eid El Fitri Mwaka huu Rais Dr.John Pombe magufuri alimtaka Mufti Sheikh Abubakar zubeir kuunda Chombo cha kubaini mali zote za bakwata zilizouzwa au kumilikiwa na wajanja wachache ili zirejeshwe mikononi mwa baraza hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni