
Hillary Clinton amesema kuwa
anasikitika kuwa aliwataja mashabiki wa mgombezi wa Republican, Donald
Trump, kama kundi la watu wasiostahili heshima.
Hata hivyo alisema kuwa ataendelea kukebehi watu wenye madharau ubaguzi wa rangi.
Meneja Mkuu wa kampeni wa Bwana Trump alikuwa amemlaumu Bi Clinton kwa kile alichokitaja kama matusi dhidi ya mamilioni ya raia wa Marekani aliposema kuwa wale wanaomwunga mpinzani wake walikuwa wabaguzi wa rangi, wapinzani wa kijinsia, maaduni wa wapenzi wa jinsia moja na wanaochukia Waislamu.
Chanzo; Bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni