Mwanamke mmoja amekuwa mtu wa kwanza katika Umoja wa Falme za kiarabu kuwasilisha ombi la kutaka kubadilishwa jinsia chini ya sheria mpya inayohalalisha upasuaji wa kufanyia mabadiliko sehemu za siri .
Wakili wa mwanamke huyo Ali al-Mansouri ameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba siku zote mteja wake amehisi kuwa yeye ni mwanamume, na amekuwa akipokea matibabu ya kimwili na kiakili kwa miaka minne iliyopita.
Ameeleza kuwa hisia za mteja wake ni kwamba mwili wake haudhihirisha jinsia yake ya kweli na ni jambo lililomsababishia wasiwasi na mawazo mengi.
Mansouri ameeleza kuwa tume ya matibabu ilipendekeza kwamba afanyiwe upasuaji huo.
Sheria hiyo mpya ya afya ya Umoja wa falme za kiarabu ilioidhinishwa mapema mwezi Septemba, inaruhusu upasuaji huo kwa misingi ya matibabu.
"upasuaji huo... Unaruhusiwa iwapo ni sehemu ya matibabu kwa matatizo ya kijinsia , kama itakavyoshauriwa na tume ya matibabu itakayoundwa kwa lengo hilo," sheria hiyo inasema.
Mahakama ya Abu Dhabi itasikiliza kesi hiyo tarehe 28 mwezi Septemba.
Chanzo: bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni