Kurasa

Jumanne, 20 Septemba 2016

Basi la New Force Lapata Ajali na Kuua Watu 12 Njombe

 Basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T429 DEU baada ya kupinduka eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe.

 Wananchi na polisi wakiwa eneo la ajali.
 …Wakiendelea kuokoa watu waliokuwemo kwenye basi hilo.

Muonekano wa basi baada ya ajali.

Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T429 DEU kupinduka eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, mkoani Njombe.
Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kuamkia leo wakati likitokea  Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.

Kwa mujibu wa habari kutoka shirika la habari la taifa (Shihata) huko Njombe, kati ya watu hao 12 wanawake ni wanane akiwemo mtoto mmoja wa kike  na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa.

Katika tukio lingine la ajali iliyotokea mkoani Kilimanjaro katika msafara wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki,  imesababisha majeruhi wawili akiwemo afisa wa polisi  na mwandishi wa habari wa Shihata ambao wote wamelazwa hospitali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni