Kurasa

Jumanne, 20 Septemba 2016

Makao makuu ya upinzani yachomwa DRC

 Afisi ya chama cha upinzani iliochomwa moto
Afisi ya chama cha upinzani iliochomwa moto

Makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yamechomwa moto katika mji mkuu wa Kinshasa huku mili miwili ilioungua ikipatikana ndani yake.

Mashambulio hayo yanajiri kufuatia makabiliano ya siku ya Jumatatu kati ya maafisa wa polisi na wafuasi wa upinzani wanaomtaka rais Joseph Kabila kujiuzulu ifikiapo mwezi Disemba

Maandamano nchini DRCMaandamano nchini DRC

Ofisi ya chama kikuu cha upinzani UPDS ni miongoni mwa zile zilizochomwa mjini Kinshasa.

Upinzani umemuonya Kabila kwamba atakuwa akifanya ''uhaini'' kwa kuchelewesha uchaguzi.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba ,lakini upinzani unahofia kwamba rais anataka kuuahirisha kwa lengo la kutaka kusalia madarakani.

Bado hajatoa tamko kuhusu mipango hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni