Mtu aliyekuwa akitafutwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu katika miji
ya New York na New Jersey amekamatwa baada ya kushambuliana na polisi
kwa risasi.
Ahmed Khan Rahami, mwenye umri wa miaka 28 ni raia wa Marekani mwenye asili ya Afghan.
Alijeruhiwa katika mapambano hayo yaliyosababishwa kukamatwa kwake karibu na nyumba yake kwenye mji wa New Jersey.
Katika operesheni ya kumkamata mtuhumiwa huyo polisi wawili pia walijeruhiwa.
Meya wa mji wa New York, Bill de Blasio amesema kuna kila sababu kuamini kwamba shambulio hilo lilikuwa ni ugaidi.
Kwa upande wake Rais Barack Obama amewataka watu kuwa watulivu
chanzo: bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni