Kurasa

Jumamosi, 17 Septemba 2016

Conte Aweka Wazi Sababu Za Kupoteza Mchezo Dhidi Ya Liverpool Jana

Antonio Conte amekiri kwamba kukosekana kwa John Terry ndio sababu kubwa ya kupoteza mchezo wa jana Liverpool.

Magoli ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Dejan Lovren na Jordan Henderson yaliwahakikishia Liverpool ushindi wa mapema ugenini Stamford Bridge.

Diego Costa alifunga goli pekee la kufutia machozi kwa Chelsea na kufuta aibu ya kuondoka kapa nyumbani..

“Nadhani tulikosa muunganiko mzuri kutoka kwa Terry: mipira ya free-kick, na kurusha ni lazima ipewe umakini mkubwa,” Conte alisema baada ya kuulizwa kama kukosekana kwa Terry kulikuwa pengo kubwa.

“Kipindi cha kwanza lazima niwe mkweli, tulicheza ovyo hali iliyopelekea kuruhusu magoli mawili.

“Unaporuhusu magoli kwenye mchezo mkubwa kama huu dhidi ya Liverpool si rahisi hata kidogo kurudi mchezoni.

“Hii ni miongoni mwa michezo migumu na nadhani unatakiwa uwe na umakini mkubwa kila wakati uwapo uwanjani, kwasababu kila kitu kinachofanyika kinaleta utofauti.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni