Msanii wa muziki, Harmonize (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete.
Wimbo ‘Matatizo’ wa msanii wa muziki Harmonize, ni moja kati ya nyimbo ambazo zinapendwa na Rais Mtaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.
Wiki moja iliyopita Mh.Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwaalika viongozi wa WCB pamoja na wasanii wake nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana.
“Unajua wakati Mh Jakaya Kikwete anatoka madarakani Diamond Platnumz bado alikuwa hajasaini wasanii wengine chini la WCB Wasafi, hivyo tulikwenda kuwatambulisha kina Harmonize, Raymond pamoja na Rich Mavoko pia na kukabidhi kazi zao, lakini uzuri wakati tunakabidhi kazi Mh Jakaya Kikwete alikuwa amevutiwa na wimbo wa Harmonize wa matatizo, akawa anasema alikuwa kwenye gari aliisikiliza kazi hiyo na kusema kuwa kijana ameimba sana,” Sallam alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.
Sallam alisema hatua ya kukutana na JK wanaimani itawasaidia kuwapa connection katika muziki wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni