Sehemu ya picha zikimuonesha mwanamuziki Diamond akiwa na Felician Mutakyawa.
Meneja Sallam kutoka WCB kupitia akaunti yake ya Instagram ameonyesha baadhi ya nyaraka ambazo zimewapitia kibali cha kutumia sehumu za wimbo ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli kwenye wimbo mpya wa Diamond, ‘Salome’.
Wimbo ‘Maria Salole’ wa Saidi Karoli ni miongoni mwa nyimbo za asili zilizofanya vizuri miaka ya 2000 na bado unaendelea kupendwa hadi sasa.
Kupitia akaunti yake hiyo meneja huyo ameandika;
“Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome.”
“Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania.” Amesititiza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni