UNAFIKIRI TECNO MPYA INAYOTARAJIWA KUTOKA HIVI KARIBUNI INAWEZA KUWA SIMU
NYEMBAMBA KUSHINDA ZOTE?
Mwezi wa 9 (Septemba)
ukiwa ukingoni kuelekea mwezi wa 10 (Oktoba) hali imekuwa ikipamba moto huku
TECNO Phantom mpya ikiwa mbioni kuzinduliwa.
Wakati tangazo
rasmi likitarajiwa kutolewa mwezi Septemba mwaka huu (2016), yote yamebaki kuwa
fununu tu kama ushahidi ikifananishwa sawa na kupigilia msumari kichwani. Swali
lililobaki ni, TECNO Phantom 6 au 6+ itabaki kuwa smartphone nyembamba kushinda
zote?
Tukiwa bado
hatuna picha kamili juu ya muonekano wake halisi, makisio yamebaki kuwa ya
kubahatisha tu. Binafsi, nasubiri kwa hamu uzinduzi rasmi wa toleo hili. Kwa
fununu na uvumi unaosambaa kuna uwezekano Tecno Phantom 6 ikawa ndio smartphone
nyembamba kutengenezwa?
Kama fununu hizi ni za kweli, swali
linabaki kuwa, ni vipi wameweza kufanya hivyo?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni