Muandishi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia....
.....Rahabu akapunguza mwendo wa pikipiki na agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda kibopa,rahab akapita njia aliyo kwenda muntar.Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi....
Edndelea....
.....Rahab akanyanyuka haraka,akamtazama muntar ambaye alianza kucheka kwa dharau akimtazama rahab kuanzia juu hadi chini.Muntar akarusha gongo kwa kutumia nguvu nyingi,rahab akalikwepa na kurusha teke lililotua shingoni mwa muntar na akaayumba,kabla hajajiweka sawa rahab akampiga muntar ngumi kadhaa za kifua na kuzidi kumfanya muntar kuyumba mithili ya mtu aliyelewa kwa pombe za kienyeji.(mataputapu).
Ilipoishia....
.....Rahabu akapunguza mwendo wa pikipiki na agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda kibopa,rahab akapita njia aliyo kwenda muntar.Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi....
Edndelea....
.....Rahab akanyanyuka haraka,akamtazama muntar ambaye alianza kucheka kwa dharau akimtazama rahab kuanzia juu hadi chini.Muntar akarusha gongo kwa kutumia nguvu nyingi,rahab akalikwepa na kurusha teke lililotua shingoni mwa muntar na akaayumba,kabla hajajiweka sawa rahab akampiga muntar ngumi kadhaa za kifua na kuzidi kumfanya muntar kuyumba mithili ya mtu aliyelewa kwa pombe za kienyeji.(mataputapu).
Muntar
akajaribu kurusha ngumi ila rahab akafanya maamuzi ya haraka katika
kuudaka mkono wake wa kulia,akajigeuza na kwakutumia bega lake akauvunja
mkono wa muntar.Kilio cha maumivu makali kikamkumba muntar.Pasipo kuwa
na huruma rahab akampiga mtama muntar na kumfanya aliachie gongo
alilolishika.Rahab akaliokota gongo na kuanza kumpiga muntar gongo la
kichwa hadi damu nyingi zikaanza kutoka nje kwa kasi kama bomba la maji
lililo pasuka sehemu ndogo.
Kibopa akafunga breki za miguu yake baada ya kukutana uso kwa uso na agnes.Kibopa akameza funda kubwa la mate huku mwili wake ukimtetemeka kiasi kwamba akabaki akiwa hajajua nini la kufanya.Agnes akaachia tabasamu pana baada ya kuiona surulia ya kibopa ikianza kuchora ramani ya kutota kwa mikojo aliyo shindwa kuizuia.
“ni....Iisssa...Mehe”
Kibopa alizungumza kwa kigugumizi kikali,agnes akapiga hatua hadi alipo simama kibopa na akamtisha kama anampiga ngumi ya uso,kwa woga uliokithiri ukammdondosha kibopa chini kama mzigo na akaanza kulia kama mtoto mdogo
“khaa wewe si jambazi,mbona unalia sasa?”
“mimi ni nilikuwa kibaraka waoo tuu,sioooo jambaazzziiii” kibopa alizungumza kwa kuyavuta vuta maneno kama amemeza fumba la uji wa moto na anashindwa kuumeza.Agnes akamtazama kwa huruma kipopa ambaye taratibu alianza kupiga magoti akimuomba msamaha.Agnes akampiga kofi la shavu kipopa na kumuamuru kusimama
“wenzenu wapo wapi?”
“wameshakufaa”
“changanya mbaliga zako,kabla sijabadilika”
“eheee....!!”
Agnes akampiga kibopa teke la makalio huku akimsindikiza na kofi la mgongoni na kumfanya kibopa aanze kukimbia kwa kasi kubwa.Agnes akabaki kucheka kwani hakutarajia kama ataweza kukutana na mwanaume muoga kama kibopa.
*****
Jackson luther mpelelezi anaye sifika kwa kazi yake nzuri akaanza kupandisha ngazi kwenda juu alipo anna kwa lengo la kumtia nguvuni kwa kosa la mauaji.Anna akaanza kukimbia akipandisha ngazi kwa kasi hadi akafika alipo waacha wezake.
“tuondokeni kimenuka”
Wakasaidiana kumkokota fety ambaye amechoka sana kwa kazi ya kupambana na karim pamoja na shamsa.Wakaingia ndani ya lifti na kushuka hadi gorofa ya kwanza,jackson akaitoa bastola yeka na kuwa makini zaidi,taratibu akaanza kuuunguza mwili wa muntar na kuhakikisha kwamba uhai wa mwili huo umesharudi kwa Mungu baba.
Kitu
ambacho kinamchanganya jackson luther ni juu ya nani aliyeweza kumuua
karim kwani ni miongoni mwa majambazi ambao alijaribu kuwafuatilia kwa
kipindi kirefu pasipo kupata mafanikio ya aina yoyote katika kazi ya
uchunguzi wake.Akapandisha hadi gorofa ya tano alipomuona anna
akimalizikia na akakuta korido ikiwa haina mtu hata mmoja.
Akachunguza sehemu yote na kumkuta mtu aliye anguka chini akiugulia maumivu na mlango wa kuingilia chumbani kwake ukiwa upo wazi, akamsogelea na kumpa mkono na kumuinua kutoka alipokuwa.
“umepatwa na nini?”
“kuna wadada bwana hapa,walikuwa wakipigana na kuniangusha”
“umeumia?”
“ndio nimepiga kiuno chini.”
“wameelekea wapi?”
“hata sijui wametoka vipi humu ndani kwangu”
“sawa”
Anna,fetty na halima wakaingia kwenye jiko kuu la kupikia vyakula kwa kutumia mlango wa chini wakashuka kwenye ngazi na kutokezea upande wenye maswimcming pool katika hotel,wakawatizama watu waliomo ndani ya hotel na kuona hakuna anayewatilia mashaka kwa mwendo wa umakini wakaanza kuelekea kwenye sehemu lilipo gati la kuingilia hotelini.Kabla ya kutoka nje ya geti walinzi wakawasimamisha,kwa jicho la kuiba fetty kwa kupitia kioo cha dirisha la kijumba cha walinzi akaona video inayomuonyesha akipambana na shamsa kupitia kwenye tv ndogo iliyopo kwenye kijumba cha walinzi
*****
Rahab alipo hakikisha amekipasua kichwa cha muntar kwa kukipiga magongo,akatafuta sehemu chini ya mti na kukaa huku akiyasikilizia maumivu makali ya kifua aliyopigwa kutokana na kupigwa gongo.Agnes akaanza kumtafta rahab na kwabahati nzuri akamkuta akiwa amekaa chini ya mti
“shost umempata huyo mjinga?”
“ndio”
“umemuua?”
“hapana,nimemuachia aende zake kwa maana nimeona hana hatia.”
“mpumbavu kweli wewe,unadhani atashindwa kwenda kujipanga na kuja kutudhuru?”
“atatupatia wapi?”
“wewe mjinga nini?” rahab alizungumza kwa hasira kubwa.
“mpumbavu mwenyewe unadhani kila mtu ni wakumuua,mtu gani huna roho ya huruma”
“ila kumbuka ni nini tulichoamua”
“si tumesha kamilisha kama ni muntar kufa umesha muua,sasa kwa nini damu nyingine zije juu yetu pasipo kuwa na sababu ya msigi”
“katika siku ambazo ag nikuona kuwa wewe ni mjinga,limbukeni,poyoyo ni leo”
Rahab aliendelea kuzungumza kwa dharau iliyo changanyikana na hasira kali
“mimi poyoyo si ndio?” agnes alizungumza kwa hasira
“ndio wewe poyoyo”
Agnes akamsukuma rahab na kumfanya rahab kunyanyuka kama mbogo mkali aliye punyuliwa na risasi,akamrukia agnes kwa kutumia teke lake na kumuangusha agnes chini.Agnes akampiga mtama rahab na kumuangusha chini,wakaanza kushikana nywele zao na kuanza kuminyana huku wakipiga piga kelele.
“rahab nitakuua”
“niue kama unaweza”
Agnes akamuachia rahab nywele na akasimama.Rahab akamtazama kwa jicho kali agnes na akachia msunyo mkali
“rahab hebu tuache maswala ya kitoto,sisi ni marafiki kitu kinacho tufanya haswa tugombane ni nini?”
“wewe si ndio mzembe,unafanya vitu vya kijinga”
“sio vitu vya kijinga,kuna mambo yakufanya na mengine sio ya kufanya.Hivi rohoni mwako unaroho gani hadi umuue mtu asiye ha hatia”
“agnes hebu mtazame yule mjinga alivyokuwa akitumiminia risasi,unadhani angetuua ingekuwaje?”
‘ila haijawa,cha msingi tufanya mpango turudi tunapo ishi”
Agnes akampa mkono rahab na kumnyanyua,wakauvuta mwili wa muntar na kuuficha kwenye kichaka.Agnes akaikagua pikipiki na kukuta haijaharibika sana zaidi ya kuvunjika kioo cha pembeni cha upande wa kushoto.Agnes akaiwasha pikipika na rahab akapanda kwa nyuma na kuondoka porini na kutokea barabara kuu iendeyo mikoani na safairi ikaendelea
*****
“hamruhusiwi kutoka humu ndani”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akiwazuia anna,fetty na halima wasitoke,wakaongezeka walinzi wawili wakasimama mbele yao huku mikononi wakiwa na bunduki zao
“kwa nini,huturuhusiwi kutoka?” anna aliwahoji
“kwa sababu maalumu.Tunawasubir......”
Fetty hakumuacha mlinzi kumaliza sentensi yake,akamtwanga kichwa kilichomfanya mlinzi kuishika pua yake iliyoanza kuvuja damu.Kwa shambulio hilo walinzi wengine wakawa wameduwaa kumuona mkubwa wao akivujwa na damu.Anna na halimwa kwa utaalamu mkubwa wakawapokonya walinzi bunduki zao,
“polisi”
Sauti ya jackson luther ikasikika kwa nyuma ikiwaamrisha fetty na wezake kutulia kama walivyo huku akiwa ameishika bastola yake kwa umakini.Anna akageuka kwa haraka na kufyatua risasi moja iliyompiga jackson luther kwenye paja la mguu wa kushoto na kumfanya aanguke na bastola ikaangukia mbali na alipo.
Mlinzi
mmoja akajaribu kumrukia halima ila risasi ya bunduki iliyotua tumboni
mwake ikamfanya arudishwe nyuma na kuanguka kama mzigo wa kuni.Macho ya
jackson luther yakatazama na macho ya anna akajaribu kuunyoosha mkono
wake kwenye bastola yeka ila akastukia risasi nyingine ikitua kwenye
mkono wake na kumfanya jackson luther kutoa ukulele mkali wa maumivu.
Fetty akamvuta kwa haraka askari aliye mpiga kichwa na kumchomolea bastola iliyopo kiunoni mwake.
“waamrishe wezako kutufungulia geti”
Fetty akamvuta kwa haraka askari aliye mpiga kichwa na kumchomolea bastola iliyopo kiunoni mwake.
“waamrishe wezako kutufungulia geti”
Fetty alizungumza huku bastola akiwa ameielekezea kwenye kichwa cha mkuu askari wa hoteli,akawaamrisha wezake waliopo kibandani na wakalifungua geti linaloendeshwa kwa umeme.Wa kwanza kutoka akawa ni halima,akawaamuru watu waliomo ndani ya gari la kifahari aina ya range rover linalo ingia kwenye hoteli.
Vijana
wawili wa kiarabu waliomo ndani ya gari wakashuka na kulala
chini.Halima akaingia na kuwasubiria fetty na anna ambao nao wakingia
kwa na kuondoka hotelini wa kasi,gari mbili za polisi zilizokuwa
zinafika hotelini baada ya kupigiwa simu na wasamaria wema zikaanza
kuwafukuzia kwa nyuma.
Wakiwa ndani ya gari fetty akatoa simu na kumpigia dokta willim huku akizitazama kwa nyuma gari za polisi zinazo kuja kwa kasi
“vipi kazi imekwenda vizuri?”
“ndio ila kuna tatizo limetokea”
“tatizo gani?”
“tumezidiwa ng............”
“vipi kazi imekwenda vizuri?”
“ndio ila kuna tatizo limetokea”
“tatizo gani?”
“tumezidiwa ng............”
Fetty hakumalizia sentesi yake na akajikuta akijigonga kichwa kwenye kioo na gari yao ambayo ilikumbwa na lori la kubebea mchanga ambalo halima ajiribu kulipita kwa kupitia upande wa kushoto kinyume na sheria za barabara,gari ikaanza kuserereka ndani ya mtaro kwa kasi ya ajabu kwa ubavu wa kustoto aliopo fetty na kugonga kwenye karavati la barabara na kusababisha gari kuminyika minyika vibaya sana na gari moja ya polisi ikamshinda dereva wake kuwahi kufunga breki na ikajikuta ikiligonga lori kwa nyuma na kupenya chini ya uvungu wa lori na kusababisha askari wote sita waliopo ndani ya gari,miili yao kugawanyishwa vipande viwili..................
ENDELEA NAYO KUPITIA ubuyublog.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni