Nikupe changamoto leo wewe unayetafuta ajira. Kabla haujatuma maombi ya
kazi jiulize wewe kama wewe unaweza kuifanyia nini kampuni au asasi
husika ? Je una ujuzi gani haswa au ni mambo gani haswa unaweza
kuyafanya ambayo yatakua ya muhimu katika hiyo kampuni au asasi
unayofikiria kuomba nafasi ya kazi ?
Kumbuka muajiri haajiri CHETI chako, haajiri CHUO ulichosoma.
Anachohitaji haswa NI WEWE KAMA WEWE na hali yako ya kujituma, kufikiria
, na utayari wako wa kuingiza kitu katika asasi husika.
Jipime mwenyewe kwa kuanza hivi: Nenda kwa website ya asasi au kampuni
husika, kama hawana website basi omba vipeperushi au maandishi yoyote
yanayoelezea kampuni au asasi husika. Soma kuhusu shughuli zao, bidhaa
zao, muundo wao wa uongozi, malengo yao, changamoto zao n.k.
Kisha jilinganishe wewe kwa ujuzi wako , nini unaweza kufanya ktk
uzalishaji wa hiyo asasi, nini unaweza ongezea katika usimamizi, jiulize
wewe kama ndio ungekuwa mfano meneja wa masoko ungefanya vitu gani
tofauti, au wewe ndio ungekuwa computer programmer wa hiyo asasi au
kampuni ungetengenezaje website au apps zenye kuiboresha hiyo asasi n.k
La msingi ni kuwa kabla haujaomba kazi katika asasi au kampuni husika
jiweke ndani ya hiyo asasi au kampuni halafu jione kwa kiwango gani una
fiti na kuwa wa muhimu.
Kama ukijipima wewe mwenyewe na kujiona haufikii basi jiulize wapi ktk ujuzi wako, wapi ktk sifa nyingine unahitaji kuongeza.
Chanzo:Muungwana.co.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni