
Waziri wa habari Sudan Kusini
amesema kuwa serikali haitajibu madai ya ripoti mpya inayodai kuwa
viongozi wa nchi hiyo wananufaika kutokana na vita vya wenyewe kwa
wenyewe vinayoendelea nchini humo.
Michael Maquei Lueth amesema
kuwa serikali ina mambo mengi ya kusema kuhusu madai hayo lakini
itafanya hivyo ikiwa itapatiwa rasmi taarifa za kina.Ripoti iliyosimamiwa na muigizaji wa Hollywood na mwanakampeni George Clooney inadai kuwa Rais Salva Kiir,kiongozi wa upinzani Riek Machar na mkuu wa jeshi pamoja na familia zao wanafaida zinazofanana.
Inawaunganisha wasomi wa Sudan Kusini katika mchezo wa fedha unaojumuisha nyumba za kifahari, migodi ,mafuta na kampuni nyengine.

Image caption Vita hivyo vilivyoanza 2013 vimedhoofisha uchumi wa nchi
Chanzo Bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni