
Rais wa Zambia Edga Lungu ameapishwa hii leo baada ya kuchaguliwa tena wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti.
Kuapishwa kwake kunafanyika baada ya upinzani kushindwa katika kesi ya kutaka matokeo ya uchaguzi kubatilishwa.
Bwana Lungu alishinda uchaguzi wa tarehe 11 mwezi Agosti kwa asilimia 50.35 na kupita kiwango kilichokwa kuepuka kurudiwa tena kwa uchaguzi.

Mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema alishindwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi mahakamani
Hakainde Hichilema ambaye alichukua nafasi ya pili kwa asilimia 47.63 anaendelea kupinga matokeo hayo.
Mwandishi wa BBC aliye kwenye uwanja wa National Heroes katika mji mku wa Zambia Lusaka, anasema kuwa takriban watu 60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Edga Lungu.
Chanzo: bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni