Moto huo ulisambaa kwa haraka katika nyumba hiyo ya ghorofa nne Watu ishirini wameuwawa nchini Bangladesh katika moto mkubwa katika kiwanda kimoja, uliosababishwa na mlipuko wa kifaa cha kuchemsha maji.
Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa viungani mwa mji mkuu Dhaka, na inaarifiwa kwamba huenda idadi ya walioaga ikaongezeka.
Polisi wanasema kwamba zaidi ya watu 100 walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho, na kwamba moto huo ulisambaa kwa kasi katika jengo hilo la ghorofa nne.
Wazima moto wakiwabeba waathiriwa kwenye ajali hiyo ya motochanzo bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni