Maafisa wa korea kusini wametahadharisha kwamba huenda Korea Kaskazini
ikafanya jaribio jingine la bomu la nyuklia wakati wowote, baada ya
kutekeleza jaribio jingine la bomu la nyuklia Ijumaa.
Jaribio hilo la Ijumaa lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Korea Kaskazini.
Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema bado kuna shimo la kulipua bomu
ambalo halijatumiwa katika eneo la kufanyia majaribio Punggye-ri ambalo
linaweza kutumiwa kulipua bomu la sita wakati wowote.
Korea Kaskazini ilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa baada ya
jaribio hilo la Ijumaa na hali ya wasiwasi na uhasama imeongezeka.
Jumapili, mmoja wa maafisa wa jeshi la Korea Kusini alinukuliwa na
shirika la habari la taifa hilo Yonhap akisema kwamba nchi hiyo ina
mpango wa kuuangamiza kabisa Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini,
iwapo kutaonekana dalili kwamba nchi hiyo inajiandaa kutekeleza
shambulio la kinyuklia.
Bado kuna shaka kuhusu uwezo wa Korea Kusini kuweka mabomu ya nyuklia
kwenye makombora ya masafa marefu, kuiwezesha kutekeleza shambulio,
lakini wataalamu wanasema hatua zilizopigwa na taifa hilo zinazua
wasiwasi.
Jumatatu, shirika la Yonhap lilimnukuu afisa mmoja wa serikali akisema
dalili zinaonesha Korea Kaskazini imekamilisha maandalizi ya kutekeleza
shambulio jingine milimani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni