WAZIRI
wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed, amesema
haridhishwi hata kidogo na kusuasua ya ujenzi wa jengo jipya la baraza
la mji Chakechake Pemba, linalojengwa na kampuni ya Nowe Investment Co
LTD ya Tanzania bara.
Alisema
ukarabati na ujenzi unaofanyika kwa ofisi ya baraza la mji Mkoani
unaridhishwa, ingawa kwa ujenzi wa jengo hilo la Chakechake hali imekuwa
sio ya kuridhisha na kumtaka mjenzi kuhakikisha anakuwa makini kwenye
kazi zake.
Waziri huyo alitoa tamko hilo jana wakati alipokuwa akizungumza na mhandisi mjenzi wa kampuni hiyo, kwenye jengo hilo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku tatu kisiwani Pemba ya kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Alisema
alitarajia sana kampuni za kizalendo zionyeshe umahiri na ukakamavu
wanapopewa kazi, ingawa kwa kampuni ya Nowe Investment, kazi yao kwenye
jengo hilo hairidhishi.
Aidha
Waziri huyo wa fedha alimueleza mjezni huyo kuwa lazima sasa waongeze
idadi wa watendaji kazi (vibarua) na kuhakikisha wanaongeza muda wa
kazi, ili jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati mwafaka.
Alifafanua
kuwa kama kipindi cha mkataba wa awali kimeshapita bila ya
kulikamilisha, lazima sasa waheshimu na wathamini miezi mitano
waliopewa, katika ujenzi wa jengo hilo.
Aidha
aliongeza kuwa, sio busara kwa kampuni zenye makao makuu yake Tanzania
bara, wakubwa kujifungia huko na kuwaacha vibarua wakiendesha ujenzi.
“Sasa
kama mmeomba miezi mitano mengine sawa, lakini na nyinyi acheni
kujifungia Tanzania bara, kuweni kwenye kazi zenu muda wote, ili
mkamilishe kazi kwa wakati’’,alifafanua.
Mapema
Mhandisi wa jengo hilo kutoka kampuni hiyo Elmeka A. Shuma, alisema
kulikuwa na mambo kadhaa yaliosababisha kutokamilisha ujenzi huo kwa
wakati, ikiwemo kuchelewa kupewa uamuzi baada ya kuomba jambo.
“Muheshimwa
waziri tukikaa miezi zaidi ya mitatu, twangoja tujibiwe kama tuvunje
ujenzi wa awali au laa, lakini hata uwekaji wa jamvi kupewa jawabu nako
kulichelewa”,alifafanua.
Kwa upande mkandarasi wa jengo hilo na ukarabati
wa jengo la baraza la mji Mkoani, Joseph Maradu kutoka kampuni ya Mekon
Consultant Engineering, alimueleza Waziri huyo kuwa kutokuwa makini kwa
baadhi ya kampuni za kizalendo ndio tatizo.
“Mimi
naona kuchelewa kwa jengo hili la ofisi ya baraza la mji Chakechake,
kwa baadhi ya kampuni za kizalendo kutokuwa makini na kazi zao na
kujisahau’’,alifafanua.
Awali
Waziri huyo wa fedha na ujumbe wake, ulitembelea pia ujenzi wa barabara
ya Ole –Kengeja yenye urefu wa kilomita 35 barabara ya Mgagadu –Kiwani
yenye uref wa kilomita 6.3, zoezi la ununuzi wa karafuu kituo cha Mkoani
na Hospitali ya Abdalla mzee Mkoa
Chanzo; zanzinewz.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni