Choo kilichotengezwa na dhahabu
Raia wako huru
kutumia fedha zao kidogo ili kupata huduma ya choo kilichotengezwa na
dhahabu katika jumba la makumbusho la Guggenheim.
Msanii kutoka Italy,Maurizio Cattelan alijenga choo hicho kwa kutumia carat 18 za dhahabu na kukiita choo hicho Marekani.
Choo hicho cha maonyesho kimewekwa katika msala wa kuogea wa Guggenheim kulingana na the New Yorker.
Jumba hilo la makumbusho limekitaja choo hicho kuwa kazi nzuri.
Choo hicho cha dhahabu kilijengwa katika choo chengine kinachotumiwa na jinsia zote mbili.
Wageni wanaolipa kiingilio cha jumba hilo la makumbusho wataweza kukitumia wanavyotaka.
Choo kilichotengezwa na dhahabu
Choo hicho kinalenga kuwapa fursa raia wa tabaka la chini kujifurahisha katika mandhari ambayo hutumiwa na matajiri pekee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni