WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka za serikali za mitaa nchini
kuweka haraka majina katika barabara na mitaa katika maeneo yao, ikiwa
ni sehemu ya utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi.
Waziri
Mkuu pia ameelekeza taasisi za serikali kuzipa kipaumbele kwa Manispaa
ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma
wakati wa kutekeleza mpango huo.
“Dodoma
na Chamwino ndio yawe maeneo ya kipaumbele wakati wa kutelekeza mradi
hiyo kwani serikali imeshabainisha nia yake ya kuhamisha mji mkuu wa
nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma,” amesisitiza.
Waziri
Mkuu Majaliwa ametoa maelekezo hayo jana wakati wa Uzinduzi wa Muongozo
wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa
mjini hapa pamoja.
Amewataka
mawaziri na mamlaka husika kukamilisha kuweka majina ya mitaa na
barabara ifikapo Desemba, mwaka huu. Amezitaka taasisi za umma na
binafsi, kuweka kipengele cha anwani za makazi ili kutekeleza mpango huo
wa maendeleo.
Alizitaja
taasisi hizo kuwa ni pamoja na Wakala wa Barabara wa Tanzania
(Tanroads), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Shirika la Taifa la Nyumba
(NHC) na Mipango Miji na Mradi wa Kuboresha Miji. Alisema mpango huo
mpya utaboresha mpangilio wa miji, utasaidia masuala ya ulinzi na
usalama, huduma za kijamii na kuboresha mazingira ya biashara na uchumi
nchini.
“Itakuwa rahisi kukusanya kodi za serikali kwa sababu itakuwa rahisi kutambua na kufuatilia walipa kodi katika maeneo yao," amesema.
Mpango
huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Posta ya Mwaka 2003 na
Azimio la Umoja wa Posta Duniani (UPU) lililofikiwa Doha, Qatar mwaka
2012, lililotaka nchi zote duniani kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa na
anuani. Kamu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Christine Mndeme alimhakikishia
Waziri Mkuu kuwa mamlaka za Dodoma, zimeanza kutekeleza mpango huo wa
kuweka anuani katika mitaani na kwenye barabara za mji huo mkuu.
“Mpango
wetu Dodoma ni kuipa mitaa na barabara majina ya viongozi waliohai na
waliokwishafariki kutokana na mchango wao hapa nchini kama vile Pius
Msekwa, Job Lusinde, Hayati Rashid Kawawa na George Kahama,” alisema Mndeme.
Nchini
Tanzania mradi wa majaribio, ulianzia Mkoa wa Dar es Salaam na Arusha
na baadaye ulifuatia Mkoa wa Dodoma na mpango ni kukamilika Juni, 2018.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni