Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, amemuapisha
aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Ramadhani
Kitwana Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.
Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania
nchini Malaysia Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wakati huo huo, Rais Dk John Pombe Magufuli, amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.
Walioapishwa ni Eliya Mtinangi Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa
kwanza wa Mkoa wa Songwe ulioanzishwa rasmi Mwezi Februari 2016 mwingine
ni Adoh Stephen Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.
Mwingine aliyeapishwa ni Tixon Tuliangine Nzunda anayekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Rukwa ambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies
Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.
Baada ya kuapishwa, Balozi Dau na Makatibu Tawala wote watatu wamekula
Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na
Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na kushuhudiwa na Rais
Magufuli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni