Dodoma. Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari
Mbabala, Manispaa ya Dodoma, Helena Mpondo amejifungua mtoto ndani ya
bweni.
Mwanafunzi huyo amejifungua mtoto mwenye afya njema kwa usaidizi wa
walimu na baadaye aliitwa mganga wa zahanati ya jirani kwa ajili ya
kumkata kitovu na msaada mwingine.
Helena, Ijumaa ya Septemba 2 saa tatu asubuhi alizidiwa na uchungu akiwa
peke yake bwenini, lakini matroni na mwalimu mwingine wa kike waliwahi
kufika eneo hilo na kumsaidia kujifungua salama.
Mkuu wa shule hiyo, Joram Mkwawa amesema siku ya tukio, saa tatu asubuhi
aliitwa na walimu wenzake bwenini na alikuta binti huyo amejifungua.
“Nilichofanya niliwaambia waende zahanati na nilituma pikipiki ya
kumfuata mzazi wake ambaye alipofika, nilimkabidhi mwanawe kwa kuwa ni
kosa kukaa na mtoto mwenye mimba,” amesema.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme
alitoa taarifa kuwa manispaa hiyo ilikuwa na wanafunzi 51 wenye mimba na
kati yao, 45 walikuwa wa shule za sekondari na sita wa shule za msingi.
Chanzo;Muungwana.co.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni