ABIRIA wa mabasi ya kwenda mikoani na nchi jirani katika Kituo
cha Ubungo (UBT), wa- natozwa viingilio batili kiny- ume cha utaratibu.
Utaratibu unaojulikana abiria anapokuwa na tiketi hairuhisiwi kumtoza
fedha za kiingilio ambayo ni Sh 300. Hata hivyo, hali ni
tofauti kwani watu wote wamekuwa wakitozwa fedha za viingilio.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, abiria hao walisema
wameshangazwa na utaratibu huo,kwani siku zote wanaposafiri
huingia katika kituo hicho kwa kutumia tiketi za mabasi
wanayosafiria.
Mmoja wa abiria hao Angela Yoredi aliyekuwa akisafiri kuelekea
Dodoma na basi la ABC alisema ilimpasa kulipia kiingilio cha Sh
200, licha kuonesha tiketi yake mlangoni.
“Nashangaa imebidi nilipie Sh 200 wakati siku zote nikiwa na tiketi ya
basi ninapita bila kulipia, waliniambia huo ni utaratibu mpya
unaotumika kwa sasa,” alisema Angela.
Naye Mohamedi Issa ambaye alikuwa anasafiri na basi la Hood
kwenda Morogoro alisema kwa sasa utaratibu wa kuingia
katika kituo hicho haueleweki, kwani awali watu waliokuwa
wanalipa ni wale waliokuwa wakiingia kituoni kwa ajili ya kupokea
au kusindikiza abiria.
“Utaratibu wa humu sasa haueleweki pale mlangoni kuna abiria wanalipa
Sh 200 lakini mimi nililipa Sh 300 in- gawa nilikuwa tayari na
tiketi yangu ya basi,” alisema.
Akitoa ufafanuzi wa suala hilo, Ofisa Uzalishaji, Uratibu na Ushuru
kituoni hapo, Novat Francis, alisema kitendo hicho ni kinyume cha
sheria na uta- ratibu ambao umepangwa katika kituo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni