Kurasa

Alhamisi, 15 Septemba 2016

Paroko wa Kanisa Katoliki Ulumi, Awachapa Fimbo Waumini Kwa Kulidharau Kanisa Katoliki

Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Ulumi jimbo la Sumbawanga Fr Peter Twamba ameawaadhibu kwa kuwatandika viboko mbele ya altare na mbele ya waamini Wasabato wanne kwa madai ya kulidhalilisha kanisa Katoliki.

Wasabato hao waliingia kanisani RC kujumuika na wakristo, wakaomba waweze kuwasalimia wakiristo, walipopewa nafasi kipindi cha matangazo wakasema kuwa _"sisi ni wasabato wa siku ya saba halali, jumapili siyo siku ya kusali Bali siku ya kwanza ya Juma. Wakasema kuwa ninyi mnaosali siku ya jumapili mumepotea"_ wakacharazwa viboko
bonyeza linki hii kuona video; https://youtu.be/NWCbOdVSoZc

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni