Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ameunga mkono uamuzi wa Rais John
Magufuli kuahirisha safari kwenda nje ya nchi ili kushiriki katika maafa
ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Kikwete amesema uamuzi huo ni wa busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kushughulikia tatizo hilo.
Kikwete aliyemtumia salamu za pole Dk Magufuli na waathirika wa tukio
hilo, amesema misaada ya haraka na dharura inahitajika ili waathirika
waendelee kupata huduma zote muhimu hasa za kibinadamu.
Kiongozi huyo mstaafu ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya
nyumba 22 za watumishi wa afya, 10 zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na
nyingine 10 Mafia zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani
Pwani.
“Ndugu zangu pamoja na leo hii tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa
afya mkoani kwetu, naomba tusimame tuwakumbuke wenzetu waliopoteza
maisha katika tetemeko la ardhi huko Bukoba na pia natumia fursa hii
kutoa pole kwa waathirika wote na Rais Dk Magufuli,” amesema.
Ameongeza kuwa: “kiukweli amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili kushiriki katika maafa haya.”
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.
Chanzo" muungwana.co.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni