Mwanamuziki na muigizaji nchini, Snura Mushi, ameamua kujipa cheo cha
Malkia wa Uswazi pasipo kujali ya kuwa yupo mwanamuziki mwenzake, Shaa,
ambaye kuanzia hapo awali alikuwa akijiita kwa jina hilo.
eNewz ilimtafuta Snura na kupiga naye story kuhusu kujiita 'Malikia wa
Uswazi' suala ambalo Snura alisema yeye amekulia kwenye maisha ya
Uswahilini (Uswazi) na hata nyimbo ambazo anaziimba zina maudhui ya
mazingira ya uswahili hivyo hata akijiita ni sahihi.
“Mimi nimeandika vile nikiamini kuwa mimi ni malkia wa uswazi, kwanza
nimekulia huko nimekaa huko na hadi sasa hivi bado nakaa huko na nyimbo
zangu pia ni za uswazi so sioni kama kuna shida nikijiita malkia wa
uswazi.” Amesema Snura Mushi.
Hata hivyo eNewz bado iliendelea kumuuliza kuwa inakuwaje Shaa akisikia
kuhusu yeye kujiita malkia wa uswazi lakini Snura bila uoga alisema mimi
najiamini na sijali mtu atachukuliaje kuhusu hilo kwa sababu hata
mashabiki nao wananiita malkia wa uswazi mara malkia wa kisingeli so
sioni shida na hayo yote ni kutokana na muziki wangu na maisha yangu
kiujumla.
“Mimi sijali kwamba mtu atachukuliaje kwa sababu hata mashabiki nao
wananiita hivyo tena sasa wameongezea kuwa mimi ndio malkia wa kisingeli
pia hayo yote ni kutokana na mziki ninaofanya na mwisho wa siku watu tu
wenyewe wanajua tu nani malkia wa Uswazi”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni