Msanii Diamond Platnumz alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya
East Africa Radio wiki kadhaa zilizopita alifunguka na kusema kuwa
katika maisha yake toka ameanza kuwa na mahusiano na Zari hajawahi
kumsaliti.
Diamond Platnumz anasema kuwa moja ya sababu kubwa kwa yeye kutomsaliti
mpenzi wake huyo kwanza ni kwa sababu wanaonana mara kwa mara lakini
kingine alidai kuwa kazi ya muziki siku zote inamfanya kuwa 'busy'
kuhangaika na muziki hivyo hapati nafasi hiyo ya kuhisi anaweza
kumsaliti mpenzi wake huyo.
"Mimi sijawahi kusaliti, kweli kabisa bado sijapangiwa nadhani lakini
unajua mimi na Zari tunaonana mara kwa mara kwa kuwa nasafiri sana na
huwa nina waambia watu kama Zari angekuwa anakaa Tanzania asingepata
muda mzuri wa kukaa na mimi, kwa kuwa nasafiri sana kwa sababu za kikazi
hivyo hata angekuwa Tanzania ningekuwa napishana naye, unajua masuala
ya muziki yana stress sana kila siku unawaza nyimbo, unawaza video mara
unatakiwa usimamie kazi za Harmonize atengeneze video kali, uhakikishe
Rayvanny atengeneze ngoma kali mara Rich Mavoko aweze kuwa mkubwa zaidi
kwa hiyo unakuwa kuna vitu vingi unavitazama hivyo unakosa muda wa
mapenzi. Kwa mfano siku mbili nzima nimelala WCB sijalala nyumbani kwa
ajili ya kazi za muziki." alisema Diamond Platnum
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni