Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliokimbilia nchi jirani sasa
imefikia milioni moja, wakiwemo 185,000 waliokimbia mzozo mpya ulioibuka
jijini Juba mnamo July nane mwaka huu, limesema Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.
Kwa mujibu wa UNHCR, idadi hiyo inatia Sudan Kusin katika orodha ya nchi
zenye mizozo iliyosababisha wtu zaidi ya milioni moja kukimbia nchi zao
ambazo ni Syria, Afghanistan na Somalia.
Mapigano kati ya wnajeshi wanaomtii Makamu Raisi wa zamani Riek Machar
na jeshi la serikali ya Sudan Kusini yamelazimisha maelfu kukimbia
makwao hivi karibuni, huku zaidi wa milioni 1.61 wakisalia kama
wkaimbizi wa ndani.
Uganda ndio imepokea idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan Kisini
ikiwa na takriban laki nne ikifuatua na Ethiopia yenye wakimbizi 292,000
na Sudan inayohifadhi 247,317.
Wakati huohuo, UNHCR, imetoa ombi la 80% ya dola miloni 701 za
kutekeleza operesheni zake za za kushughulikia wakimbizi wa Sudan Kusini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni