Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara amesema, kikosi kimejiandaa vizuri
kwa ajili ya kuweza kupambana na wanauchukulia huo kama michezo mingine
hivyo wanaamini wataweza kuvuna pointi tatu mbele ya Azam FC.
Manara amesema, mpaka sasa wana majeruhi wawili pekee ambao ni
mshambuliaji Ibrahim Ajibu na kiungo Mwinyi Kazimoto ambao daktari
anaendelea kuangalia hali zao kama wataweza kucheza mchezo wa kesho au
bado wataendelea kuwa katika uangalizi.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Azam FC Jafary Iddy Maganga amesema,
mchezo huo utakuwa na changamoto kubwa kutokana na wote kuwa na pointi
sawa katika msimamo wa ligi lakini watapambana ili kuhakikisha
wanashinda huku akiwataka waamuzi wa mchezo huo kusimamia sheria 17 za
soka ili kuhakikisha timu inashinda kutokana na uwezo wake.
Maganga amesema, kwa upande wao majeruhi ni walewale ambao walikuwa nao
katika mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ni mshambuliaji Gonazo Bi
Thomas, Beki Erasto Nyoni na Agrey Morris pamoja na Mlinzi wa kati
Paschal Wawa.
Michezo mingine itakayopigwa hapo kesho ni Mtibwa Sugar wakiwakaribisha
Kagera Sugar Uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro, Mbeya City
akiwakaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya, Mwadui
FC akiikaribisha Yanga Uwanja wa Mwadui Mjini Shinyanga na Ruvu Shooting
akiikaribisha Mbao FC Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni