JESHI
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limeahidi kuwachukulia hatua kali
wananchi wanaotumia vibaya simu za dharura, zenye namba 111 na 112.
Simon
Sirro, Kamishina wa Jeshi la Polisi amesema kuwa watu wamekuwa wakipiga
simu hizo na kutoa taarifa za uongo au kupiga simu na kisha kuwapa
watoto wadogo waongee.
“Polisi
tutawafuatilia wote kupitia mitandao yetu General Packet Radio Service
(GPRS),inayoonyesha maeneo walipo na simu wanazotumia ili kuwakamata na
kuwachukulia hatua kali za kisheria. Haiwezekani mtu apige simu halafu
baada ya simu kopokelewa anaweka muziki,” amesema.
Kamanda
Sirro amesema ni vyema wananchi wakaacha mzaha na matumizi ya namba
hiyo ya Jeshi la Polisi kwani kwa kufanya hivyo inapunguza morali ya
askari wa jeshi hilo kufanya kazi kwa kujituma.
“Wananchi
wote watumie simu zetu kutoa taarifa zenye ukweli na zitafanyiwa kazi
kwa wakati, wawasiliane na sisi pale wanapoona viashiria vya uhalifu ama
tukio lolote linaloleta uvunjifu wa amani na siyo kupiga simu na
kufanya mzaha,” amesema Sirro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni