Majagina wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, KULIKO JANA, uliopo kwenye santuri yao ya tatu: Live and Die in Afrika.
Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa
uaminifu wa Mungu haukomi kamwe. Huruma yake haiishi – kila uchao ni
vipya.” Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo
mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umezikwea chati na kuwagusa mashabiki
barani Afrika na zaidi.
Video maarufu ya Sauti Sol wakiimba akapela ya wimbo huo wakiwa na
Redfourth Chorus, ulivutia masikio ya watu mashuhuri duniani na kwenye
vyombo vya habari hadi kumfanya Amber Riley, nyota wa kipindi
kilichoshinda tuzo za Emmy, Glee, kuandika kwenye Instagram, “Sielewi
wanachokisema lakini najua ni kizuri. Inasikika kimalaika, kuna yeyote
anayejua kama kuna video?” Mastaa wengine waliowahi kuiweka video hiyo
kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja Master P, Anthony Hamilton, Jb
Smoove na WorldstarHipHop, miongoni mwa tovuti zingine za habari za
kimataifa.
Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya KULIKO
JANA, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mweye kipawa cha hali ya
juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki. Sauti Sol wamesema kwenye
taarifa yao, “KULIKO JANA ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na
safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu
ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”
Video ya KULIKO JANA imetayarishwa na Fulfillment Limited, na
kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi. Wimbo
umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol. Kipande cha akapela kilipangwa
na Philip Tuju na Redfourth Chorus.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni