Kurasa

Jumatano, 14 Septemba 2016

USIPUUZE KILA KITU NA USIAHIRISHE KILA KITU



Mgonjwa mmoja aliyelazwa hospitalini alitembelewa na ndugu zake. Alikuwa amewekwa kwenye mashine ya oksijeni na hivyo hakuweza kuongea.
Wakati wakiwa pembezoni mwa kitanda, mgonjwa huyo alichukua kalamu na kipande cha karatasi akaandika ujumbe na kumpatia mmoja wa ndugu hao ambaye alikiweka mfuko bila kukisoma huku wakiendelea na mazungumzo.
Baada ya dakika chache, mgonjwa alifariki dunia. Ndugu yule aliingiza mkono mfukoni mwake ili kujua marehemu aliandika nini. Wajua nini kilichotokea? Kwa masikitiko ujumbe ule ulisomeka hivi:
“Tafadhali sogea pembeni kidogo, umekanyaga mpira wa oksijeni. Siwezi kupumua tena, unaniua”.
FUNZO:
Je, unaahirisha kusoma ujumbe? Je, unapuuza kupokea simu kwa sababu anayekupigia tayari wamjua? Huwenda ujumbe unaochelewa kuupokea ni muhimu kwako au kwa mtu mwingine ambaye yuko katika wakati mgumu.
Tafadhali pokea simu na usome ujumbe unaotumiwa. USIAHIRISHE KILA KITU.
Usisome ujumbe huu peke yako, usambaze kwa marafiki na jamaa zako

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni