Kurasa

Jumatano, 14 Septemba 2016

HAYA NDIYO MASHARTI YA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI KWA ANAYETAKA KUMUOA DADA YAKE



Kim Yu Jung (29) dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jung Un, amekuwa mwanamke namba moja nchini humo baada ya kuteuliwa kuongoza kamati kuu ya chama tawala mwezi huu.
Kaka yake, bwana Kim (33) anamtafutia dada yake mume, na yeye ndiye atakayeendesha zoezi la kuwapima vijana 30 maridadi wa Pyongyang.
Mwaka 2012 utawala wa nchi hiyo ulijaribu kumtafutia mume, lakini hawakumpata anayeendana na matarajio yao, na sasa kazi hiyo inaanza tena baada ya binti huyo kupata cheo kikubwa baada ya mkutano mkuu wa saba wa chama ambao ulifanyika mwezi huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.
Mtu anayetaka kumuoa binti wa kiongozi wa Korea Kaskazini lazima awe mhitimu au mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kim Il Sung, na awe na urefu wa zaidi ya sentimeta 175, awe na muonekano mzuri na awe amemaliza mafunzo ya kulitumikia jeshi.
CHANZO: #Mzizima24

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni