Beki wa Chelsea John Terry amerejea mazoezini baada ya kupata
majeraha yalimweka nje kwa takriban wiki moja na nusu na anatarajiwa
kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya mahimu wao Arsenal
utakaopigwa Jumamosi wikiende hii.
Nahodha huyo wa Chelsea aliukosa mchezo wa nyumbani waliofungwa magoli
2-1 dhidi ya Liverpool Ijumaa baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu
kwenye mchezo ulioisha kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea
.
Nohodha huyo wa zamani wa England hatacheza mchezo wa Kombe la EFL dhidi ya Leicester utakaochezwa leo usiku.
Meneja Antonio Conte amesema: ‘Tumesikitishwa sana na kipigo dhidi ya
Liverpool lakini nashukuru tumerekebisha makosa yetu na nimeona ari
waliyonayo vijana mazoezini. Ni suala zuri sana.
‘Ni wiki ngumu hii kwasababu tunaenda kupambana na timu mbili kubwa.
Leicester walishinda ubingwa msimu uliopita na Arsenal ni timu kubwa
ambayo inawania ubingwa msimu huu. Ni wiki ngumu hii lakini tuko
tayari.’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni